MWAMBE AMEPEWA TUHUMA ZA KUTAKA KUMUUA MKUU WA JESHI LA POLISI!
Aliyekuwa Waziri katika Serikali ya Tanzania, Mhe. Geoffrey Mwambe ameachiwa huru jana kabla kesi ya kulitaka Jeshi la Polisi limpeleke mahakamani leo kusikilizwa.
Kwa mujibu wa wakili wake, Hekima Mwasipu; Mhe. Mwambe anatuhumiwa kwa tuhuma kuu mbili ambazo ni:
1. Kutaka kumuua Mkuu wa Jeshi la Polisi, ila Jeshi hilo halijataja jina Mkuu huyo ambaye Mhe. Mwambe inasemakana alitaka kumuua.
2. Uchochezi wa kimtandao. Jeshi la Polisi pia halikutaja ni uchochezi upi huo ambao Mhe. Mwambe alikuwa akifanya mtandaoni.
Jeshi la Polisi lilimuachia jana kwa dhamana ya Polisi ikiwa ni siku kadhaa kupita tangu Mhe Mwambe apoteze. Kelele za mitandaoni ndizo zililiibua Jeshi la Polisi kukiri kuwa liko naye na pia kesi dhidi ya Jeshi hilo ndilo imepelekea limuachie huru.
Tuendelee kupaza sauti kwa ajili ya Lucy Shayo anaywshikiliwa Kituo cha Polisi Chang'ombe kwa siku kadhaa bila kufikishwa mahakamani. Lakini wako mamia ya watu wengine ambao wanashikiliwa katika vituo vya polisi katika nchi nzima bila tuhuma zao kueleweka.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 15 Desemba 2025; Saa 7:25 adhuhuri