Sasa maji ya Ziwa Tanganyika kutumika kwa wananchi wa Jimbo la Kavu Wilaya ya Mpibwe Mkoani Katavi

Sasa maji ya Ziwa Tanganyika kutumika kwa wananchi wa Jimbo la Kavu Wilaya ya Mpibwe Mkoani Katavi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
SEKTA YA MAJI YABAINISHA DHAMIRA YA KUTUMIA MAJI YA ZIWA TANGANYIKA MKOA WA KATAVI

Mpwimbe-Katavi

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amesema Serikali imeshatangaza tenda kwa ajili ya kumpata mhandisi mshauri atakayefanya tathmini ya kutoa maji ya Ziwa Tanganyika yaweze kutumika kwa wananchi wa Jimbo la Kavu Wilaya ya Mpibwe Mkoani Katavi.

Waziri Aweso amebainisha hayo wakati wa Ziara ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu aliposimama kuwasalimia wananchi wa Kibaoni Wilayani Mpimbwe ambapo ameeleza kuwa wizara ya maji haitakuwa kikwazo kuwapatia wakazi hao huduma ya majisafi kwa ajili yamatumizi ya majumbani na Kilimo.

Aidha Mhe. Aweso ametumia wasaa huo kumuagiza Mhandisi wa Maji wa Mkoa na Wilaya kuhakikisha ndani ya wiki mbili wananchi waishio katika eneo la uchima wanapata huduma ya majisafi na salama.

Katika hatua nyingine Waziri Aweso ameelekeza ifikapo kesho wataalamu wafike katika eneo la Kavuu Mahali alipozaliwa Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda kwa ajili ya kuchimba kisima ikiwa ni sehemu ya kuboresha huduma ya maji katika eneo Hilo.

Pia soma: Jinsi ziwa Tanganyika lilivyo na maji mengi
 
Back
Top Bottom