Mshangazi mdogomdogo
Member
- Sep 23, 2024
- 64
- 43
Kumbe neno fake news lina maana tofauti na wengi tuelewavyo. Inatolewa taarifa yenye ukweli ila Kama anayetakiwa kuwajibika hasipokuwa tayari kuzungumzia inaitwa fake news ,wanaibatilisha na kuwaaminisha watu kuwa ni habari ya uongo wakati ina ukweli. Mfano hii ya wanafunzi mkoa wa Ruvuma kukaa chini ni taarifa yenye ukweli Kuna Shule Za msingi wanafunzi wanakaa chini tena hapa manispaa ya Songea sijui hali ilivyo huko pembezoni mwa mkoa ,.ila bila uoga mtu mwenye manufaa binafsi anasema ni fake news. Kuna Shule Za msingi watoto wetu wanakaa chini na hatuoni jitihada zozote zinazochukuliwa, bila aibu mnapinga ukweli wakati tunaojionea hali ilivyo tunavyoenda kwenye vikao vya Shule kuhimizwa kuchangia Pesa ya chakula basi ipitishwe rasmi moja ya michango Ni mzazi kuchangia Pesa ya dawati au mwanafunzi aende na dawati .Mtoto tangu chekechea hadi anafika darasa la tano hajawahi kukaa kwenye dawati alafu mnasema fake news.
Tunaomba Raisi wetu mama Samia ingilia Kati tuma timu yako ijionee Hali ya uhitaji wa madawati ilivyo, maana inaonesha hata nawe unapewa taarifa Za uongo.
Tunaomba Raisi wetu mama Samia ingilia Kati tuma timu yako ijionee Hali ya uhitaji wa madawati ilivyo, maana inaonesha hata nawe unapewa taarifa Za uongo.