Byendangwero
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 871
- 56
Kwa maoni yangu, miongoni mwa kasoro kubwa zilizomo katika rasimu ya pili ya katiba, ni kupuuzia kutaja 'usawa wa binadamu,' kama mojawapo ya tunu za taifa. Jambo la ajabu, ni kwamba watu wengi hawaoni kama kutowekwa kwa dhana hiyo ya usawa kama ni kasoro kubwa. Hii ina maana kwamba watu wengi sasa wanakubali kuwa kuendelea kukua kwa pengo ya walionacho na wale wasiokuwa nacho ni halali kabisa! Kama hivyo ndivyo ilivyo, naanza kuwa na mashaka juu ya mustakali wa nchi yetu, kwakuwa haiwezekani watu wachache wahodhi uchumi wa nchi yetu wakati wengine wamedidimia kwenye dimbwi la umasikini halafu pawepo amani.