Jicho la Tai
JF-Expert Member
- Oct 10, 2012
- 1,450
- 600
Katika pitapita zangu nimekutana na video inayoonyesha jinsi sisi wajasiliamali tunavyoweza kujisajili mtandaoni na kuomba mikopo ya Halmashauri. Bila shaka hatutasikia tena nakala kupotea au vikundi hewa. Nimefurahishwa na usajili kutumia namba ya NIDA na siyo majina hewa kama tulivyokuwa tunasikia.
Nimeingia mikopohalmashauri.tamisemi.go.tz nimeona kweli unafunguka.
Kama kweli mfumo huu utasimamiwa vyema basi hili ni suluhisho tosha la kupunguza malalamiko yetu ya kunyimwa mikopo na pengine kucheleweshewa kwa sababu mbalimbali, hata tukienda ngazii za juu kulalamika wataona ushahidi kwenye mfumo. Narudia kama kweli mfumo utasimamiwa na ngazi zote, basi ule urasimu wa awali sasa hatutakutana nao.
Ombi: Serikali ihakikishe kweli mifumo inatumika, siyo sasa tukienda tunaanza kuambiwa mfumo unasumbua. Hili jibu la mfumo unasumbua ni la kuzoeleka sana Halmashauri, yaani ukienda kufuatilia jambo wanasingizia mfumo. Bahati nzuri kwa huu, ukiniambia hivyo nami naingia kwenye simu yangu naangalia.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI ILIYONIFUNGUA MACHO.