Napitia mtandaoni Kenya, naona joto la siasa limepanda na kufikia pakubwa.
Sasa majibizano yanayoendelea, mikutano inayofanyika, polisi wanavyofanya sasa ni dhahiri nchi ipo kwenye kampeni za 2022.
Ndoa ya Uhuru na Ruto inaning'inia kwa uzi mwembamba sana sasa. Wanasiasa wa upande wa Ruto wanamshambulia Raila na Uhuru na BBI, huku wa ODM wakijibu.
Kambi ya Ruto sasa hivi wamekuwa kama ndio wapinzani japo wapo chama tawala, huku ODM wakiwa kama wapo serikalini.
Siasa za Kenya ni tamu sana, kama upo kwenye movie.