Nadhani Issue si Kupinga Matokeo Mahakamani; Jombo la Muhimu na la maana zaidi ni Kuwa na Tume huru ya Uchaguzi ambayo itakuwa mwaarubani ya Kutokwenda mahakamani.
Kwa maana hata mahakani Unapokuwa umeporwa haki unaweza pia kuwakuta walewale walioshiriki kukupora haki, na hili kwa Tanzania hii si geni. Tumeona Wajanja Wachache "ESROW GUYS"Wanavyojificha kwenye Vifungu vya Kisharia Kuhusu zuio la Kesi mahakama. Hivyo Mahakama Si Kimbilio la Waporwa haki.
Tume huru ya Uchaguzi, Isiyokuwa na Wateule wa Chama Chochote Cha Siasa Inaweza Kutuvusha salama October, 2015; Bila tume huru ya Uchaguzi Wapinzani Kushika Dola ni Doto za Mchana na pia Inaweza kutuletea Mshikemshike maana maanadalizii ya kambi zote Ktk Kulinda kura na Kusimamia uesabuji na utangazaji wa matokeo Zimejiandaa Vya kutosha.
Tunawaona Green guards na Pia Blue guards wako Kikazi zaidi this time around.Lakini Pia ile Kauri ya Wapigwa Tu inaendelea Kushika kasi kadri tunavyokaribia Kufanya maamuzi ya mambo muhimu ya Taifa hili.