kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,634
- 7,015
Wote wenye hoja ya serikali tatu naamini walizingatia kutokuzitonesha hisia za, na utashi wa wazanzibari ambao wamekuwa wakionyesha kupitia viongozi wao kutoridhishwa na aina hii ya muungano wa serikali 2.Hakuna mtu wa bara anayelakamikia muungano uliopo zaidi ya kujibu kejeli na matusi yanayotolewa kwa watu wa bara kutoka kwa baadhi ya wazanzibari wakiamini eti watu wa bara(Tanganyika)wanawabana katika muungano huu kiasi kwamba zimekuwepo kauli mbiu kama "mtuache tupumue" "tunataka turuhusiwe kujiunga na OIC kwani 99% ya wakazi wa Zanzibar ni waislamu"Watu wa bara makafir na mna roho mbaya!kwa nini hamdai Tanganyika yenu?!Sisi wengine tunashangaa tu kwa vile tunajua matatizo tuliyonayo si kwa sababu ya muungano ila kutowajibika kwa watawala ambao huchangia kudidimiza maendeleo yao wakishirikiana na wanyang'anyi wa nje ya nchi wenye majina matamu kv.wawekezaji!Sasa kwa vile inaonekana serikali 3 ni nongwa na wengi kwa unafiki wanataka tubaki na serikali 2 ili, kwanza kuepuka gharama(sababu nyepesi) na, pili kuepusha kuvunja muungano(Hoja isiyo na mashiko)Basi pamoja na hoja zao dhaifu tukubali lakini,Ili kuepuka kabisa hofu ya hayo wanayosema kwenye hoja zao,waunge mkono kuundwa kwa serikali moja na serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar ivunjwe.Zanzibar kama bara kuwa na mawaziri wakuu ama magavana wawili chini ya rais mmoja wa JMT
Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums