Karibu sana kwenye mkutano wetu wa kuchagua viongozi.
Vitendo SACCOS Inawaalika Wapenda Maendeleo Wote
Update...
Wadau,
Kwanza tunashukuru AlhamduliLlah mkutano umeenda vizuri na umeisha salama.
Tunafuraha kuwafahamisha wadau wote kuwa mkutano umeenda vizuri kabisa na umefana sana.
Tulianza kwa kukaribishwa na Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Vitendo...
Kisha nikaongea kidogo mimi kuwakaribisha wajumbe wote...
Baada ya hapo ikaanza semina ya ushirika iliotolewa na Afisa Ushirika wa wilaya ya Kibaha, Bwana Msangi. Semina ilikuwa ndefu kidogo lakini ilitoa mwangaza mpana wa nini SACCOS, vipi iongozwe, nini haki za Wana SACCOS na vipi haki zao zinalindwa na kusimamiwa na sheria rasmi za vyama vya ushirika na vipi serikali inasimamia vyama vya ushirika.
Yalizuka maswali mengi kiasi na hususan lilipoongelewa suala la kuendesha saccos kwa riba.
Hatimae kila mtu akaelewa kuwa hakuna tatizo kubwa isipokuwa ni namna tu ya mfumo wa uendeshaji SACCOS bila riba utavyofanyika.
Hilo na mengine yaliojiri mtajionea mkanda wa video.
Baada ya semina ukaanza mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa muda. Ulioendeshwa na kusimamiwa na Afisa Ushirika kama sheria zinavyotaka.
Hatimae tukapata kamati ya uongozi wa muda ya uanzilishi wa Vitendo SACCOS Ltd., kwa mujibu wa Sheria na chini ya usimamizi wa Afisa Ushirika wilaya ya Kibaha.
Kamati hio ya muda ikamteua Katibu wa kwanza wa muda wa Vitendo SACCOS Ltd., chini ya usimamizia wa Afisa Ushirika wilaya ya Kiabaha.
Mambo yote hayo yapo kwenye video na picha. Zitakapokuwa tayari, tutapandisha video YouTube na kwenye tovuti yetu (inayoanadaliwa kwa sasa) tutapandisha video na picha.
Tunakaribisha maswali.
Asanteni na karibuni kujiunga na Vitendo SACCOS Ltd. kwa faida ya wengi.
Abdul Ghafur
Mwenyekiti
Mobile / Whatsapp 0625249605