Sasa Tunaanza kuulizana Kwa vipi uwanja huu ni mali ya CCM?

Sasa Tunaanza kuulizana Kwa vipi uwanja huu ni mali ya CCM?

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801


Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora.



Sehemu ya ndani ya uwanja huo.
  • Habari ambazo ninazo kutokana na kuhoji wakazi kadha wa kadha wa mkoa wa Tabora, uwanja wa Ally Hassan Mwinyi ni mali ya chama tawala CCM. Lakini nilipohoji ni nani aliyeujenga uwanja huo nikaambiwa ulijengwa na mkuu wa mkoa huo wa zamani hayati Lawrence Gama ambapo baadhi ya bidhaa ziliongezwa bei kidogo ili kupata fedha za kuujenga uwanja huo mpaka hapo ulipofikia. Sasa kwa maelezo hayo machache inamaanisha uwanja huo ni mali ya wakazi wa mkoa huo na si CCM kama ilivyo sasa, au labda tungeambiwa unamilikiwa na serikali ya mkoa wa Tabora ingeeleweka. Na tatizo hili halipo Tabora tu bali hata Dar es Salaam, ambako pana majengo mengi Chama kimejigawia likiwemo la umoja wa vijana pale mtaa wa Lumumba na Morogoro rd na yale yote ya umoja wa wanawake na taasisi nyingine znazomiliki majengo. Chama kilijigawia rasilimali hizo pale Tanzania ilipoingia katika mfumo wa vyama vingi, lakini sioni pana mantiki gani wajimilikishe huku mali hizo zilikuwa za vijana wa Tanzania sio wa CCM. Na wapiga kelele sijapata kuwasikia wakilizungumzia hili. Wadau anayelijua vizuri suala hili tafadhali anieleweshe pengine wana uhalali wa kumiliki majengo hayo.
 
Back
Top Bottom