Sasa umeshakuwa upumbavu; Akilawiti shehe wakristo wanachekelea, akilawiti padri waislamu wanachekelea!!

Sasa umeshakuwa upumbavu; Akilawiti shehe wakristo wanachekelea, akilawiti padri waislamu wanachekelea!!

Status
Not open for further replies.

NIMEONA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2019
Posts
3,862
Reaction score
5,693
Ndo hali halisi humu jukwaani sasa!

Hakiangaliwi chanzo tena, ikitokea habari ya kubaka/kulawiti basi watu hukimbizana kuangalia kwanza nani katenda na si ilikuaje au tatizo nini hadi limetendeka hilo. Akishajulikana tu mbakaji/mlawiti (kiimani) basi watu hukimbizana tena mbio za speed ya hali ya juu kuja humu kuwahi kukashfu upande wa imani anayotokea mbakaji au mlawiti. Yaani hakuna anayehangaika na nini chanzo cha kuongezeka kwa haya mambo na tiba yake ya kudumu ni ipi bali hangaiko linakwenda kwenye ushindani wa ukali wa kashfa atakayoweza kuitoa mtu. Huu upumbavu kabisa!!

Kwa upumbavu huu, walawiti na wabakaji wanakuwa entertained kulingana na upande wanaotokea na, kama laana tunayolipwa kutokana na huu upumbavu, wanaongezeka kila leo. Watoto hawako salama tena, haijalishi wanatokea upande gani wa imani.

Ni wakati wa kuacha upumbavu sasa.
 
Ugm bin champion huyu jamaa sijui ana matatizo gani kichwani.?? Ni mpuuzi ,ni mbaguzi wa hali ya juu ,anaandika upumbavu sana humu kwenye jukwaaa
 
Hii issue ya ulawiti mwanzoni watu waliichukulia kama ipo exclusively kwa waislamu tu, na kusahau ulawiti ni kitendo na sio imani ya mtu. Sasa kutokana na kuongezeka kwa uwazi katika kanisa matendo kama haya yakawa wazi kwa umma. Muslims nao wakapata points za kujitetea.

NB: Tukemee vitendo viovu na sio kukashifu imani za watu. Hakuna sehemu yoyote katika Quran au Bible inayotoa ruhusa kuhusu hivi vitendo. ULAWITI NI KITENDO SIO IMANI tujue kutofautisha.
 
Kadiri siku zinavyo songa WaTz tunazidi kuwa wapimbavu tena walio vuka mipaka sijui tumerogwa?

Na mbaya zaidi hawa waeneza chuki za kidini ni watu wazima tena wenye familia, na wana jiita wasomi ambao ukiwakutana barabarani utawaona ni watu wenye akili kumbe kichwani wame jaza upumbavu wa chuki za kidini.

Alafu kingine uongozi wa jf nao unachangia kuendekeza huu upumbavu nyuzi za kushambulia dini fulani zimeenea kwa kasi humu na ID zinazo fanya huu upuuzi zinajulikana lakini uongozi wa jf hawachukui hatua.

Huu upuuzi unatakiwa kupigwa vita kwa nguvu zote.
 
Huo ni upumbavu mkuu ambao Vatican wameweka vichwani kwetu ![emoji35]
Amkeni watanzania walahi!
 
Kinachoendelea ni chuki za kidini kuna mambo mengi tu hali hii inatokea siyo ya ulawiti/ubakaji.
 
Watanzania tunapenda ligi kweli yani.

Sometimes naonaga tunawalaum tu bure viongozi wetu maana hata sisi wananchi huku nchini amna kitu kabisa ni takataka tupu kichwani.

Navyojua akili za wanachi ndo akili za viongozi wao kwaiyo wananchi akili zikibadirika naona na viongozi akili zita change.
 
Watanzania tunapenda ligi kweli yani.

Sometimes naonaga tunawalaum tu bure viongozi wetu maana hata sisi wananchi huku nchini amna kitu kabisa ni takataka tupu kichwani.

Navyojua akili za wanachi ndo akili za viongozi wao kwaiyo wananchi akili zikibadirika naona na viongozi akili zita change.
Ndo hivo maana viongozi hawatokei mbinguni, ni watu haohao ambao tuko nao kwenye jamii, kwahio kama jamii ni utopolo basi hata viongozi nao watakua hivyohivyo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom