Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 620
- 1,240
Teknolojia inazidi kushika kasi watumiaji wa window 11 na window 10 wamewekewa mfumo Rahisi wa kuweza kuingiliana kati ya simu na kompyuta na kuweza kutumika bila shida yoyote.
Tunajua wengi mmeshawahi kutumia app ya phone link ambayo inakupa Uwezo wa kufanya mambo mbalimbali kwa kukuonyesha notification na taarifa mbalimbali za simu yako kwenye kompyuta achana na hiyo.
Sasa Microsoft wanakuletea feature mpya ambayo inafanya kazi kwa watumiaji wa window 11 na window 10 kuweza kuona vitu mbalimbali vilivyopo kwenye simu na kuvipeleka kwenye kompyuta bila kuunganisha na waya.
Utaweza kufungua file explorer utaweza kuona simu yako yote kwenye kompyuta hivyo utakua na Uwezo wa kuhamisha kitu chochote kwa urahisi bila kutumia USB waya au Phone link.
hakikisha simu yako ina support android version 11 na kuendelea Kisha ingia setting kwenye simu yako >> Bluetooth & device >>mobile device unganisha na kompyuta yako Anza kutumia.