Sasisho: Kombo Mbwana wa Tanga akosa dhamana licha ya kutimiza masharti ya dhamani kama ilivyopangwa

Sasisho: Kombo Mbwana wa Tanga akosa dhamana licha ya kutimiza masharti ya dhamani kama ilivyopangwa

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
UPDATES KUHUSU KOMBO MBWANA TWAHA, TANGA

TAREHE YA KUTAJWA KWA KESI
Leo Kesi ya Jinai namba 19759/2024 ilitwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mheshimiwa Moses Maroa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga kwa ajili ya kuja kutajwa (Mention)

MASHITAKA DHIDI YA KOMBO

Tarehe 16/07/2024 Kombo Mbwana Twaha alisomewa mashitaka matatu ikiwemo (1).kutotoa taarifa kuhusu laini ya simu,(2) kutumia laini isiyo na jina lake pamoja na (3) kutotoa taarifa ya mabadiliko ya laini ya simu.

DHAMANA
Siku hiyo hiyo ya tarehe 16/07/2024 baada ya Kombo Mbwana Twaha kukana mashitaka yake ,Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga ilisema dhamana ya Kombo Mbwana Twaha iko wazi

MASHARTI YA DHAMANA

Mahakama ilitoa masharti ya dhamana kwamba anapaswa (1) kuwa wadhamini wawili walio na (2) barua za utambulisho kutoka serikali ya mtaa na (3) watakaosaini dhamana (bond) ya milioni 2 kila mmoja.

Kesi ya Kombo Mbwana Twaha ilihairishwa siku ya tarehe 16 July 2024 na kupangiwa tarehe 30 July 2024 kwa ajili ya kuja Kutajwa.

DHAMANA YA KOMBO

Masharti ya dhamana ya Kombo Mbwana Twaha yalitimizwa kwa kuwasilisha nyaraka zilizohitajika toka tarehe 17 July 2024 na baadae tarehe 18 July 2024 na 19 July 2024 Mahakama iliandaa amri ya KOMBO MBWANA kuletwa mahakamani ili apatiwe dhamana jambo ambalo halikutekelezwa na jeshi la Polisi pamoja na Magereza.

YALIYOJIRI LEO MAHAKAMANI (30 July 2024.

Leo tarehe 30 July 2024 wadhamini wa Kombo Mbwana Twaha na mawakili wake walifika mahakamani lwa ajiki yankesi kutajwa na kukamilisha dhamana ya Kombo Mbwana Twaha

RCO APELEKA KIAPO KUZUIA DHAMA YA KOMBO

Wakili wa serikali akaieleza Mahakama kwamba amekuja na kiapo cha Kamanda wa Upelelezi Mkoa wa Tanga, ACP MANYAMA WAMBURA

kwamba katika kiapo hicho ACP MANYAMA WAMBURA anaiomba Mahakama Kombo Mbwana Twaha asipewe dhamana.

kwamba bado Jeshi la polisi wanaendela na Upelelezi na wana nia ya kuongeza watuhumiwa wengine katika kesi hiyo ya jinai namba 19759 ya mwaka 2024

MAWAKILI WA KOMBO WAISHANGAA MAHAKAMA

Upande wa utetezi uliieleza mahakama kuwa kinachofanywa na upande wa Jamhuri ni kinyume cha kisheria,

Mahakama ilishatoa masharti ya dhamana hivyo kwa kuwa Kombo ameshatimiza masharti ya dhamana apatiwe dhamana,hakuna hoja ya dhamana tena mbele ya Mahakama zaidi ya kukamilisha masharti ya dhamana yaliyotolewa na Mahakama.

kama kuna maombi yoyote kwa upande wa Jamhuri yafuate utaritibu wa kisheria sio kuleta kiapo cha RCO wakati wa sasa wa ukamilishaji wa amri ya Mahakama.

Itakuwa kumnyima haki mtuhumiwa ambae amekwisha kushikiliwa kwa zaidi ya siku 43 na kupewa dhamana kwa amri ya Mahakama.

HAKIMU MOSES MAROA ASHINDWA KUMPATIA DHAMANA KOMBO

Licha ya hoja hizo za wazi mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Tanga bado mahakama imesema itasikiliza hoja za pande zote mbili tarehe 12/08/2024

Silu hiyo Hakimu Mkazi Mwandamizi Mheshimiwa Moses Maroa atasikiliza kuhusu dhamana ya Kombo na kiapo kilicholetwa na RCO wa Tanga kisha atapanga siku ya kutoa uamuzi.

MAWAKILI WA KOMBO WAMSHITAKI HAKIMU MOSES MAROA

Mawakili wa Kombo Mbwana Twaha waliwasiliana na Mawakili wa CHADEMA Dar es saalam kwa kuchukua hatua za Kumlalamikia Hakimu Moses Maroa kwa Msajili wa Mahakama kwa kushindwa kusimamia sheria na taratibu za Mahakama.

Huku wakimtuhumu kushirikiana na Jeshi la Polisi kucheza haki za mteja wao Kombo Mbwana Twaha.

Picha ya kushoto ni Kombo Mbwana Twaha na Upande wa Kulia ni RCO -TANGA ,ACP MANYAMA WAMBURA

Pia soma:Mbwana Kombo wa Tanga, kada wa CHADEMA bado hajapata dhamana, inadaiwa Mawakili walinyimwa ushirikiano na Hakimu Moses Maroa
 
Haki na Uhuru ni mbinguni tu.

Siasa salama na mageuzi ya kweli ni kwenye nchi zilizoendelea ndizo hamna hizi mambo.

Kuna mtu alikomenti kwenye mada kuhusu Rais Ruto kuwapa nafasi wasomali, kwamba waafrika/wabantu hatupendani.

Nikakomenti shm, viongozi na wasomi wote hakuna mwenye uthubutu kutoka ktk haya yanayoendelea Afrika.
 
  • Thanks
Reactions: I M
Back
Top Bottom