Naomba nikujibu kama ifwatavyo lakini nitajibu kutokana na ulivyo uliza Mkuu
Angalizo sipo apa kebeza aina ya kuku bali najibu kutokana na uzoefu nilio kuwa nao
✓ Utagaji
Kwanza kabisa hao kuku wote ulio wataja apo juu ni chotara Yani asilimia 50 ni kwaajili ya nyama ( bloire) pia asilimia 50 ni kwaajili ya mayai ( layers) ivo chakula ndicho kitakacho amua kuku wako awe katika kundi lipi
Utagaji wa hao kuku Ina kadiliwa ni week ya 21 kwanzia kutotolewa na wastani huwa wanataga mayai mawili ndani ya siku tatu. Vitu vya kuzingatia ili kuku hao watage kwa asilimia kubwa ni
1 chakula
Ili kuku wako awe kwa ajili ya kutaga inabid apewe chakula kutokana na umli pamoja na uzito alio nao kwaiyo kwanzia
∆ 1-8 week inabidi apewe chakula chenye asilimia 18-20 ya protein
∆ 9-16 week inabidi apewe chakula chenye asilimia 16-18 ya protein
∆ 17 na kuendelea inabid apewe chakula chenye asilimia 18-20 ya protein
Siku nikipata muda nitatoa ufafanuzi jinsi ya kutengeneza chakula ili kuweza kupata izo asilimia za protein
2 kiasi Cha chakula
Kuku inabid ale kutokana na uzito wake
∆ 1-4 week inabidi apewe chakula muda wote bila kipimo masaa 24
∆ 5-8 week inabid apewe 50-90 gram kwa kuku masaa 16
∆ 9-16 week inabid apewe 95-115 gram kwa kuku masaa 16
∆ 17 na kuendelea inabidi apewe 120-125 gram kwa kuku masaa 16
3 mwanga
Kuku anavyo Anza kutaga Yani week ya 20 na kuendelea inabid apate masaa 16 ya mwanga na masaa 8 ya Giza ili Kuongeza uzalishaji wa homorne itakayo pelekea utagaji utakuwa juu
4 usafi
Banda inabid liwe safi pia vyombo vya maji na chakula inabid visafishwe
6 uokotaji wa mayai
Kuku aina ya chotara huwa wanachukua muda mrefu kwenye Maandalizi ya utagaji ivyo kama kukuwa na mayai kwenye kiota itamfanya asiwe huru kutokana na kuzuiwa na mayai ivyo inabid mayai yaokotwe mara kwa mara
✓ Magonjwa
Apo kuku wote huwa wanasumbuliawa na mangojwa ivyo chanjo na dawa ni muhimu kwa kuku wote. Mtililiko wa chanjo ni kama ufuatavyo
∆ siku ya Saba inabid uwape Newcastle kwaajili ya kideli
∆ siku ya Kumi na nne inabidi uwape Gumboro kwaajili ya Mdondo
∆ siku ya ishirini na moja inabid uwape Newcastle kwaajili ya kideli
∆ siku ya ishirini na nane inabidi uwape Gumboro kwaajili ya Mdondo
∆ siku ya thelasini na Tano inabid uwape chanjo ya Ndui Yan Flow pox
Ukizingatia izo chanjo apo juu na usafi kwenye mabanda yako Magonjwa kwako yatakuwa ni historia.
Kwa upande wa Sasso wenywe huwa awapewi iyo chanjo ya Gumboro kutokana na maelezo Yao so sitayaweka apa maana ni mambo ya biashara
∆ Kasi ya ukuaji
Hao kuku wote ukuaji wao ni sawa maana swala la ukuwaji Lina tegemeana na vitu vingi kama vile chukula, Magonjwa, Huduma kuku anazo pata pamoja na usafi wa mazingira
Lkn kwenye upande wa uzito Sasso yupo juu kuzidi wote maana yeye ni mfupi kidogo kwa kroiler
Endapo ukitaka kuku wako wakuwe haraka inabidi uwape chakula chenye asilimia 20-25 ya protein Yani ndani ya miiezi miwili wanaeweza kuwa na kilo 2.5-3.5 lkn nyama yao itakuwa sio tamu maana umelazimisha wakuwe haraka ivyo ukuaji wa tissue umelazimishwa itapelekea bahadhi ya pigment azitakuwepo ivyo nyama itakuwa ya kawaida tuu