Uchaguzi 2020 SAU kuweka wagombea wa Ubunge na Udiwani katika Majimbo na Kata zote Bara na Visiwani

Uchaguzi 2020 SAU kuweka wagombea wa Ubunge na Udiwani katika Majimbo na Kata zote Bara na Visiwani

Sauti ya Umma

Member
Joined
Aug 26, 2010
Posts
39
Reaction score
21
SAU.jpg


Chama cha Sauti ya Umma (SAU) kinakusudia kuweka wagombea katika majimbo na kata zote Tanzania Bara na Visiwani katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi oktoba 2020 (Mwaka huu).

Katibu Mkuu wa chama hicho Ndugu Majalio Paul Kyara amesema bado milango iko wazi kwa wanachama wa SAU kuchukua fomu za kuwania nafasi za ubunge na udiwani kote nchini na amewataka wanachama kote nchini hususani vijana kuendelea kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi hizo kwani dirisha bado halijafungwa.

Tunafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa kwa asilimia 100 na kwa maelezo na maulizo yoyote kila mwanachama yuko huru kupiga namba 0658270003 muda wowote masaa 24.

Kwa upande wa Nafasi ya Uraisi ndugu kyara amesema zoezi hilo lilishafungwa na tayari Mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama hicho Mheshimiwa Mttamwega Bhati Mugaywa tayari alishateuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa octoba 2020.
 
Huku ni kwa kuja, kuliko kule kwa waliotaka tuwe lock down,

sijui watanzania wangapi wangekuwa wamepoteza maisha kwa njaa

Wanasiasa wanapaswa kuangalia maslahi ya wapiga Kura wao badala ya kuangalia maslahi binafsi

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom