Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Salaam Wakuu,
Chama cha sauti ya umma (SAU) Kimezindua Kampeni na Ilani kwa Vitendo, Baada ya Kutumia Trekta kama mfano wa Jinsi Watanzania Watakavyokuwa Wanalima Pindi Wakipewa Nafasi ya Kuongoza Nchi. Wamezindua kwa kuvuna Miwa na Viazi Shambani.
Uzinduzi wa ilani umefanyika kivitendo katika eneo la KWAZOO kata ya buyuni na baadae mkutano wa uzinduzi eneo la MOMBASA karibu na stand ya mabus katika Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam.
Vipaumbele vya SAU ni;
1. Huduma ya maji Safi na salama bure
2. Eliimu mpka chuo bure
3. Matibabu bure
4. Kilimo cha kisasa nana kuwezesha kilimo hai(organic farming)
5. Kuwawezesha wakulima mikopo na kulimiwa kwa trekta bure na kuja kulipa baada ya kuuza kwasababu serikali ya SAU ita watafutia masoko ya uhakikika wakulima
6. Kutokana na migogoro mingi ya ardhi, Wizara ya ardhi itakuwa kuwa chini ya rais na Wizara zote zitakuwa 12
7. Serikali ya SAU itakuwa ya kilimo na viwanda
8. Atamteua Ummy Mwalimu na Kassim Majaliwa kuwa Mawaziri
Zaidi soma: Sauti ya Umma (SAU): Ilani ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani
Uchaguzi 2020 - Mgombea Urais kupitia SAU, Muttamwega Mgaywa na mgombea mwenza wamewasili Ofisi za NEC peku kuchukua fomu
Chama cha Sauti ya Umma (SAU) kimezindua Ilani na kampeni zake kwa ajili uchaguzi unaotarajia kufanyika Oktoba 28, mwaka huu, huku kikiahidi kuwa endapo kikishika dola huo utakuwa mwisho ma matumizi ya jembe la mkono nchini na kila mkoa utakuwa na ndege yake kwa ajili ya kubeba abiria.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ilani na kampeni za chama hicho jana, jijini Dar es Salaa, mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Muttamwega Mgaywa alisema ilani ya chama hicho imelenga kuikomboa nchi kupitia kilimo na viwanda.
Alisema chini ya uongozi wa Serikali ya SAU, hakuna mkulima atakayelima Kwa kutumia jembe la mkono, badala yake trekta ndizo zitakazotumika ili kumpunguzia mzigo kwa mkulima.
Pia aliahidi kuwa chini ya Serikali ya chama hicho, wanawake watakuwa wakijifungua bure.
Aidha, ameongeza kuwa iwapo atachaguliwa ataendeleza kazi nzuri iliyofanywa na marais waliopita hususani awamu ya tano
Kuhusu suala la ardhi na Maywa amesema kila Mtanzania atamiliki ardhi bila gharama yoyote.
Kwa upande wake mgombea mwenza wa chama hicho, Satia Musa Bebwa amewahakikishia vijana wanaomaliza elimu ya juu kupata mitaji itakayowawezesha kuingiza kipato.
Kutoka Kushoto: Mgombea urais wa Zanzibar, Issa Mohamed Zonga, Katikati mgombea urais wa Tanzania Muttamwega Bhatt Mgaywa, na Kulia mgombea mwenza Bi. Satia Mussa Bebwa
Mgombea Urais wa Tanzania kuptia SAU, Muttamwega Bhatt Mgaywa Kulia na Mgombea mwenza bi. Satia Mussa Bebwa
Wakizindua ilani Kilimo na Viwanda kwa vitendo