Ramsy Dalai Lama
Senior Member
- Apr 5, 2021
- 156
- 554
Saudi Arabia inaanza mpango kabambe wa kujenga structure ya jengo kubwa zaidi duniani kaskazini magharibi mwa ufalme huo. Muundo huo, unaojulikana kama Mirror line, kwasabab litakua la vioo na umbo lililonyooka kwenda chini kwa kilomita 170, kwa maana ukianza mwanzo wa jengo baasi ili kufika mwisho wa jengo itakubidi utembee kilomita 170. Kwa kukuwekea katika uhalisia basi jengo hilo litaanza dar na kuishia karibu na morogoro kwasabab dar mpaka morogoro ni karibu ama zaidi ya kilomita 178.
Pia majengo hayo yatakua mawili na ya vioo yenye urefu wa hadi mita 488 (futi 1,600), yakienda sambamba kwa kilomita 170 katika eneo la pwani, milima na jangwa.
Majengo hayo mawili yatakua yakitazamana kwa maana katikati ya hayo majengo kutakua ndo mtaa na kutakua na njia za kutembea kwa miguu sambamba na treni ya mwendo kasi itapita chini yake. Na inakadiriwa kuwaweka watu milioni tano ambao wataweza kusafiri mwanzo wa mtaa hadi mwisho wa mtaa wenye kilomita 170 ndani ya dakika 20 kwa treni ya mwendokasi. Pia kutakua na huduma zote za kijamii tena zitakua karibu karibu. Pia bila kusahau viwanja vya mpira pamoja na gati za meli na hata viwanja vya ndege
Project hiyo inatarajiwa kugharimu dola trilioni 1 baada ya kukamilika, pia inatarajiwa kuchukua miaka 50 kujengwa, ingawa Prince Mohammed anataka mradi huo ukamilike ifikapo 2030.
Prince Mohammed bin Salman anaamini kuwa mji huo mpya utakuwa iconic project kama ilivyo Pyramid za Misri. Kwa hiyo vizazi na vizazi hawataacha kutembelea mji huo wa ajabu