jembe la kigoma
Senior Member
- Mar 23, 2012
- 119
- 19
Ni kwa mda mrefu sasa shule,vyuo na taasisi nyingine zinazotoa huduma kwa jamii huku zikimilikiwa na makanisa hasa kanisa katoliki yamekuwa yakijidadavua kuwa na malengo ya kuwasaidia watoto na watu wasiojiweza kupata huduma wanazozitoa kwa gharama nafuu,lakini kinyume chake zimekuwa hazina tofauti na shule na vyuo vingine vinavyomilikiwa na taasisisi na watu binafsi wenye malengo ya kupata faida tu,kwa mfano kwa sasa wanafunzi wa chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino(SAUT)Wapo kwenye maandalizi ya mitihani ya kumaliza mhula(semister)ili ufanye mtihani ni lazima uwe na kadi ya mtihani,na ili upewe kadi hiyo haupaswi kuwa unadaiwa hata shilingi 500 kati ya ada ya shilingi (MILIONI MOJA,LAKIMBILI NA ELFU 32)tabu inakujakwa wale wanafunzi wanaotokea familia za kawaida,maskini na wasio na uwezo wa kuwasomesha na kugharamia gharama zingine kwa mwanafunzi,hivyo kupelekea mwanachuo kujisomesha na kuendesha maisha yake kwa kutegemea mkopo kutoka bodi ili alipe Ada,stationary nyumba na chakula,hivyo uwezekano wa kulipa ada yote bila kuacha madeni haupo,hivyo kuwanyima vibali vya kuketi chumba cha mtihani ni kuwaonea na kuwanyima haki ya msingi ya kupata elimu,kuwaambia kama haujamaliza ada wasubiri mwezi wa 9 kufanya mitihani maalumu (special)ni kwenda kinyume na lengo la kanisa kuwasaidia watoto wa maskini,hii ndo inapelekea watoto wa kike kujiuza na kupata maradhi,kama haitoshi akichelewa kulipa anapigwa faini(penati) ya shilingi laki 1,wakati huohuo chuo kinatambua kwa jinsi gani bodi ya mikopo hawaleti fedha kwa wakati hivyo kupelekea wanachuo kuishi kwa kukopakopa,wito Kama askofu mkuu Pengo alivyosema taasisi za dini zikumbuke lengo kuu la kanisa kufungua vyuo,shule na hospitali na kuwasaidia wananchi na si ufanya biashara.