Kesi kibao za unyanyasi wa kingono wanafunzi wenyewe huwa wanaogopa kutoa ushahidi. Nadhani vyuo viunde kamati maalumu za kusikiliza hizo kero za unyanyasi wa kingono kwa wanafunzi...
Kongole SAUT. Tatizo kubwa ni pale wakubwa wenyewe wanapo jihusisha na ujinga huu au wanapotaka kuwatetea watu wao.Chuo Kikuu cha Mt. Augustino Tanzania (SAUT), Mwanza kimewafuta kazi wahadhiri watatu kwa makosa ya kujihusisha na rushwa ya ngono na wanafunzi kwa nia ya kuwapa upendeleo kwenye mitihani. Chuo hicho kimesema vitendo hivyo havikubaliki na kuwataka wanafunzi kuendelea kuvifichua.
Chanzo: Swahilitimes
Kuna Vyuo kama viwili hapa hapa Jijini Dar es Salaam kama Uongozi Wao ukiiga kilichofanywa na SAUT hakuna Mhadhiri wa Kiume atakayebakia.
Kila inapowezekana vyuo vingetafuta mbinu za kutompa mhadhiri nguvu kwa kiasi hicho. Je inawezekana kwa somo kuwa zaidi ya mhadhiri mmoja? Je inawezekana kwenye research process kuwe na supervisors 2 au zaidi.Kama lectures wataendelea kuwa na 100% mandate kwa ufaulu wa mwanafunzi hata shetani akae pembeni rushwa ya ngono haiwezi kuisha.
Tudada chuoni tumekuja kuuza sura na kutamba tupo chuo halafu hatusomi......tukifeli lectures akitugusia tu ngono tufaulu wala hatunaga longolongo kuvua chupi.