Sauti ya Kamala Harris kinanda masikioni mwangu

Sauti ya Kamala Harris kinanda masikioni mwangu

bahati93

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2015
Posts
1,334
Reaction score
2,463
Wallah! sauti ya Kamala imenikosha sana, kabda akilini mwangu nilikosa sauti nzuri kutoka kwakwe nyingi ya sauti zake nilizowahi kumsikiliza nilimwona kama mtu anayeongelea puani kitendo kilichokuwa kinanikera. Sasa bwana hii Debate aliyofanya majuzi kati yake na Trump imebadilisha kabisa mtizamo wangu hasi juu ya bi mdadaa.

Yaani wana Jamii sijui niwaambie maneno gani ili muweze nielewa kinini namaanisha. sauti yake imekuwa ni kama juice ya chungwa ya baridi kwa mtu aliyebanwa na kiu jangwani. Alikuwa akipanga na kupangua mambo mazito ya taifa lile bila hata ya kupayuka. Ukisikiliza kwa umakini kuna kaukali flani hivii, ama kamejua kuninyoshea kubwa jinga lile, aga kamenikosha sana.

Na sio mimi pekee ayenibeba mzobe mzobe, hata mwamba Putin alikiri adharani jinsi anavyopendaa kicheko cha mwanamke wa Shoka.
 
ata mimi nimeona kwamba kweli trump yupo kwaajili ya kundi fulani la watu hasa wale mabillionea uyu mama ni kama nahitaji kuikoa marekani...nimependa fact and logic zake
 
Back
Top Bottom