nabii7y7
New Member
- Jun 12, 2023
- 3
- 3
UTANGULIZI
Bunge ni miongoni mwa mhimili katika mihimilimikuu mitatu ya serikali baada ya serikali na mahakama na chombo kinachofanya kazi ya kutunga sheria pamoja na kuisimamia serikali kiutendaji. Kama tunavyofahamu kuwa bunge la jamuhuri ya muungano ya Tanzania linajumuisha wabunge wa kuchaguliwa pamoja na wale wa kuteuliwa kutoka vyama mbalimbali vya siasa kulingana na wingi wa wabunge waliochaguliwa.
Katika Makala haya nitajitika zaidi kwa wabunge ambao wanachaguliwa na wananchi kwa njia ya kupigiwa kura.
Imekuwa utaratibu wa kawaida sana tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa mnamo mwaka 1992 na kushuhudia uchaguzi mkuu uliohusisha vyama vingi mnamo mwaka 1995, kuanzia hapo niseme kuwa Tanzania tukawa na wabunge mseto bungeni. Na tukatoka katika giza la nadharia chafu ya kuaminishwa kuwa upinzani unachelewesha maendeleo na kuhatarisha amani ya nchi.
Hakika tunaweza kusema kuwa nchi yetu iliweza kujikomboa sasa kutoka katika mfumo uliochangua nini kizungumzwe na kuwakilishwa bungeni, pamoja na hayo yote lakini nchi ikiingia gizani tena katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Tena kila mwenye akili timamu alishangaa kuona na kushuhudia vyama vya upinzani vilichukuliwa kama maadui wa nchi, hakika lilikuwa kipindi kigumu sana na cha kutisha katika awamu zote zilizotangulia ndani ya jamuhuri ya muungano ya Tanzania.
Sasa niende moja kwa moja kwenye mada hii kwamba Mbunge wa kuchaguliwa ndiye Mbunge ambaye wananchi tunatarajia kutuwakilisha kwa usahihi katika mhimili huu muhimu wa serikali kwa kuwa yeye ni miongoni mwa wananchi walio ndani ya chombo hiki na msemaji wa kipekee anayetambua changamoto za wananchi anaowawakilisha. Bila kujali itikadi ya dini, kabila au ukanda, Mbunge wa kuchaguliwa ni muhimu sana katika kubeba uhalisia wa wananchi wake katika kutimiza wajibu wake wa msingi kwa mpinga kura wake.
Tukiachana na ahadi nyingi wanazotuahidi wakati wa kampeni na kutokuzitekeleza kwa wakati na nyingi kujifanya kuwa wamesahau swala la msingi na kushangaza ni pale wabunge wa kuchaguliwa na wananchi wanapogeuka na kusahau kuwa wao ni wawakilishi waliobeba jamii nzima ya Watanzania ili kuilinda na kuitetea katika katika utungaji wa sheria na kuisimamia serikali kiutendaji bila kujali itikadi zao za vyama vya siasa.
Mimi binafsi naweza kusema Wawakilishi wetu bungeni wametusaliti na kugeuka kuwa wawakilishi wa vyama vyao vya siasa tu! na maslahi yao binafsi kwasababu najiuliza kila siku inakuwaje Mbunge mwenye dhamana ya kusimamia maslahi ya wananchi anaweza kuruhusu kupitishwa kwa miswada kandamizi? Kwa mfano, vipi kuhusu tozo za miamala ya huduma za kifedha kwani wakati inapitishwa wabunge walikuwa hawapo bungeni au hawakutoa maoni yao?
Maana tukiangalia asilimia kubwa ya mawaziri wanaosimamia wizara ni wabunge wa kuchaguliwa na wanafahamu uhalisia wa maisha ya wananchi wanaowakilisha.
Lakini pia licha ya hayo yote, tumeshuhudia kamati nyingi za kiuchunguzi zikiundwa na miongoni mwao huwa wabunge wetu huhusika kwa asilimia kubwa sana lakini ripoti zao zimekuwa zikikizana na maoni ya wananchi na uhalisia wa kile wananchi tunachokitarajia.
Na imekuwa kawaida kwa wabunge ambao wamepewa wizara mbalimbali yaani mawaziri kuwa na tabia ya kutoa kauli tata na za kuudhi hasa wananchi wanapolalamika kuhusu kwa baadhi ya mambo.
HITIMISHO
Katika hali kama hii mimi naweza kusema sauti ya wananchi Bungeni imesahaulika na kumezwa na maslahi binafsi ili kujineemesha wao wenyewe na familia zao.
Lakini niwakumbushe wawakilishi wetu kuwa licha ya chama chao kuwapita kugombea nafasi mbalimbali, wananchi wanabaki waamuzi wa kile wanachokiitaji.
Hivyo dhamana tuliyowapa tena sio kwa kuwalazimisha bali wao wenyewe wakituuomba tena wakati huo wakija kwetu kwa kunyenyekea sana basi wahakikishe kuwa sauti zetu zinasikika na kufanyiwa kazi ipasavyo maana hilo ni jukumu tulilowakabidhi.
Na ni vyema wabunge wetu kumbukumbu kuwa chama cha siasa siyo ngozi ya mwili kuwa huwezi kuivua maana chama cha siasa unaweza kuhama lakini uwezi kuhama wananchi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania hivyo basi chama cha siasa ni kama vazi unaweza kulivua na kubadilisha nyingine lakini mpiga kura ni kama ngozi hata ukitumia vipodozi kuibadili rangi bado itabaki kubwa mwilini mwako daima.
Nikiwa na maana ya kwamba mpiga kura wako ndio mwenye maamuzi ya nafasi yako siku zote na ni vyema kukumbuka kuwa siyo kwamba kwa kuwa umepewa nafasi ya kutuwakilishamkafikiria kubwa nyingine bora sana kuliko watu wengine bali wapo wenye uwezo mkubwa zaidi wa kuongoza kuliko nyinyi isipokuwa tu ni nafasi mmepata. Hivyo basi ni jambo jema kama mkienenda katika misingi ya utu pamoja kutekeleza majukumu yenu kwa wananchi ambao ndio waajiri wenu.

Upvote
2