Sauti ya Vijana: Nini Chimbuko la Matumizi Mabaya ya Madaraka Tanzania?

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Matumizi Mabaya ya Madaraka ni suala mtambuka linalohusisha matumizi yasiyo sahihi ya mamlaka aliyopewa mtu, au kundi fulani hasa katika nafasi ya utawala au uongozi.

Matumizi Mabaya ya Madakaraka yanaweza kuonekana katika maamuzi yanayokiuka Sheria, Kanuni au miongozo iliyopo, matumizi mabaya ya rasilimali za umma kwa maslahi binafsi au kundi fulani ambalo una maslahi nalo, pia katika ukandamizaji, upendeleo au vitendo vya rushwa.

Mara kadhaa nchini kumekuwa na Kesi walizofunguliwa baadhi ya Watumishi wa Serikali waliobainika kutumia Vibaya Madaraka yao kwa kukiuka Haki za Binadamu, Kusababisha Ubadhirifu wa Rasilimali za Umma na Kujipatia Fedha kinyume na Sheria.

Unadhani nini chimbuko la Matumizi Mabaya ya Madaraka, na nini kifanyike kupambana na vitendo hivyo?

Unaweza kushiriki katika mjadala huo utakaoendeshwa na JamiiForums Alhamisi Juni 6, 2024 Saa 12:00 Jioni hadi 2:00 Usiku kupitia XSpaces.
 
Unadhani nini chimbuko la Matumizi Mabaya ya Madaraka, na nini kifanyike kupambana na vitendo hivyo?
Chimbuko ni mfumo tu waliojiwekea hao vijana. Na kujiona miungu watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…