Sauti za Kifo Cha Mateso za Watoto, Wazee, Wanawake na Waafrika kwa ujumla zaendele kusikika kwa zaidi ya miaka 100 sasa

Sauti za Kifo Cha Mateso za Watoto, Wazee, Wanawake na Waafrika kwa ujumla zaendele kusikika kwa zaidi ya miaka 100 sasa

GuDume

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2015
Posts
6,651
Reaction score
14,337
Mpaka leo ukiwauliza waNAMIBIA kuhusiana na unyama ambao walitendewa na wajerumani miaka hiyo hasa kwa haya makabila mawili ya Herero na Nama Usishangae kwaunayemuuliza akianza kulia kwa kwikwi na kulaani akikumbuka namna babu na bibi yake, mama na baba yake walivyouawa kwa mateso makubwa jangwani huko Namibia. Mhusika alikuwa mzungu jamii ya Ujerumani. Huyu ni binadamu anayeamini yeye ndiye bora kabisa hapa duniani kuliko jamii nyingine yeyote.
namibia.jpg

Wanawake wa Kiherero. Imagine wenyewe miaka ya nyuma walikuwa wazuri hivi miaka hii wakoje? Wajerumani wakatili sana kutaka kufuta kizazi kama hiki.


KWANI ILIKUAJE?

Pembez
oni ya Nchi ya Namibia ukanda wa Pwani kuna jangwa la Namib hili lina urefu wa Mile 1,200. (Usianze kuumiza kichwa ngoja nikukokotolee) mile hizo ni sawa na kilometa 1931.213 unafika mwanza na kwendelea mbele sijui mpaka wapi. Nyuma yake kuna Milima milima na miinuko na Mashariki ukishuka utakutana na Jangwa la Kalahari. Unajua kwa Namibia kitu ambacho ni issue sana au kupat ani ngumu ni maji. Aiseee. Kule maji ni shida sana kutokana na Aina ya nchi ile ilivyo. Pia inapata mvua kiasi kidogo tu si unajua tena sababu ya Jangwa. Lakini katika udongo ule allahamdulilah kuna madini si haba… kuna uranium, tin, tungsten, copper, diamonds upande wa kusini, silver, lithium na gas asilia. Katika ardhi ya Namibia kunakaliwa na Wakulima na Wafugaji. Pia wapo Jamii ya Wahzade… yaani wale wanaoishi kwa kuwinda na kuokota. Hawalimi wala Hawafugi.

Sasa huko pia kuna makabila haya mawili ambayo ni ya wafugaji. Kuna Waherero na Wama haya ndo yalikuwa makabila makuu makubwa miaka hiyo 1840 wakati wajerumani walipoingia nchini Namibia.Kabla ya Wajerumani wazungu pekee waliokuwa wakifika huko walikuwa ni wapelelezi,wafanya biashara na mabaharia. Wakafungua biashara ya pembe za ndovu na pia mifugo. Wakaleta pia silaha n.k

Mwaka 1880 wajerumani wakaingia kusini magharib mwa afrikawakitafuta makoloni wakiwa wameongozana na Gavana ambaye yeye hakujua lolote kuhusiana na afrika. Meja Theodor Leutwein alianza kwa kuwachinganisha waherero na wama ili wakipambana wao yeye na watu wake wakae kwa utulivu wakijipanga. Baadaye wakaongezeka Zaidi na Zaidi wakiwasukumia mbali wakazi wa pale kwa kuwapa rushwa na maneno matamu matamu ya kitapeli. Na ndipo walipogundua kuna Almasi Namibia.
Leutwein01.gif

Theodor Leutwein

Wakati huo huo Hendrik Witbooi chifu wa Wama aliandika barua kwa Theodor Leutwein akimwambia kuwa wao hawajapendezwa na ule uvamizi maana wanahisi kama wamevamiwa katika ardhi yao. Alikuwa akimaini kuwa Theodor angeona jambo hilo ovu na kuwakataza watu wake wasiwanyanyase wakazi wa pale. Hayo yakiendelea Theodor akaondolewa na badala yake akaletwa Luten Jeneral Mkatili aliyekuwa akipenda sana kumwaga damu Lothar Von Trotha. Huyu jamaa ntakupatia CV yake huko mbele. Alikuja na wanajeshi wapatao 10,000 wakiwa wamejipanga tayari kabisa kwa vita wakati wowote ule.
Adrian-Dietrich-Lothar-von-Trotha.jpg

Huyu jamaa Lothar Von Trotha ukimcheck hata macho yake tu unamgundua ni katili sana

NINI KILIFUATA?

Subiri nikusimulie. Mwaka 1904-08 ni kipindi ambacho ukiwatajia ndugu zangu wa Namibia wanapatwa na uchungu sana. Kitu chenye ncha kali kinapita kwenye kifua chao kutoka juu ya moyo kinapita kushuka chini na kuacha maumivu makali sana mioyoni mwao kwa kuwakumbusha tu tukio hili la kufadhaisha, kusikitisha na kuhuzunisha sana. Miaka hiyo wakati Waafrika nao walikuwa wameshaamua kukomaa tu na vita dhidi ya wavamizi na wakoloni kila sehemu ya afrika kwa makabila madogo madogo na makubwa pia. Kila sehemu kulikuwa na harufu ya uasi. Kutoka January 1904 Wajeruman waliokuwa wakitawala Kusini Magharibi mwa Africa (Namibia) walikuwa wakikumbana na changamoto za uasi kutoka kwa wakazi wa maeneo yake kuliko ambavyo walipata kushuhudia hapo kabla.

Na hili jambo lilisababishwa na huyu jenerali roho mbaya ambaye yeye aliwaamuru waherero watoke maeneo yote oevu,yenye rutuba waende huko mbali kukavu kusiko na tija.akawambia bila masikhara kuwa asione mfugo wa mtu umesogea maeneo flan flan mazuri ambayo waligawa wao wazungu na pia sionekana mherero ana ng'ang'aa pua maeneo yale maana ameshawaambia askari zake wawalambe tu risasi.jambo hili likajenga kwaro na wenyeji ambao of course hawakupendezwa na issues hizi mpya. wakaanza kufanya choko choko na kuanza kuwashambulia wajeruman kadhaa huko huko kitaa wakikutana.

Hali hii ikawajengea Wajeruman hasira wakifanya juhudi kuzima kila aina uasi kama ambavyo ungejitokeza katika maeneo yao halafu wabaki wakila bata tu kirahisi. Tukumbuke kuwa utawala wa kikoloni ulikuwa umeshapata kibali machoni mwao wenyewe baada ya Mkutano wa Berlin mwaka 1884. Hawa watu pasipo ubinadamu walithubutu kugawana ardhi yetu kama vile watu wanavyogawana kipande cha kitambaa kila mtu akikatiwa kile ambacho angeweza kwenda kushonea kanzu au suruali.inaumiza sana. Damu mpya ya kijerumani iliyokuwa na nia ya kuji tawanya dunia nzima chini ya Mtawala William wa pili iliangalia kila sehemu chini ya dunia kuiweka kwenye himaya yake.

Lakini wajerumani walifanikiwa kunyakua maeneo machache huku afrika baada ya huo mwaka 1884 kitu ambacho kiliwapa hasara kwa sababu za gharama za kuyaendesha haya makoloni. Na pia haya makoloni yalikuwa yakionesha nguvu ya Taifa lenye kuyakalia hivyo kama unayo mengi unaonesha kuwa wewe ni taifa kubwa lenye nguvu. Namibia ikaonekana ni moja ya sehemu kwa wao kujitanua kwa sababu ya utajiri iliyokuwa nao. Walianza kwa Amani na kuamini ni shwali. Hawakujua. Hawakujua.

Mwanzo wa FIGISUFIGISU

Ni mwaka 1895 ndio hali ilianza kuwa ya mashaka na misuko suko kwa wajerumani. Kabila la Khowesi (sehemu ya kabila la khoi khoi au nama) chini ya kiongozi aliyejitanabaisha kwa ukidume Henrik Witbooi walianza kugawa kipigo kwa majeshi ya kikoloni. Kiongozi aliyekuwa mwenye mvuto kwa watu wake alitaka sana kuwaunganisha pasipo mafanikio maskini. Mwishowe aliambulia kipigo sana kwa kuwa viongoz wa makabila mengine hawakutaka kumuunga mkono katika harakati zake hizo. Kile kipigo kilijenga hofu kwa viongoz wengine wa kiafrika kupingana na wajerumani. Hapo wajerumani makatili wale wakazidi kukaza vyuma zaidi ili kuwatisha na wengine wasijaribu wasije wakaona kilicho mtoa khanga manyoya. Waliacha ujumbe kwa watu kuwa kilichomkuta Ungo na kibeku pia akijaribu kitamkuta.

Lakini bado kulikuwa na waafrika ambao hawakuogopeshwa na tukio lile. Na mwaka 1904 kabila la Herero. Hii ilikuwa ni changamoto kubwa sana kutoka kwa wajerumani. Hawakutegemea baada ya lile tukio la kumpa kipigo cha mbwa mwizi Henrik basi kuna kidume mwingine angeweza kuthubutu kuja na wazo la kuasi. Waherero walikuwa wameshaumizwa sana, wameshafedheshwa sana, wameshanyanyasika sana, wameteswa sana na utawala wa kijerumani. Maana waliona liwalo na liwe kama noma na iwe noma hawakubali nao wanataka ku revenge. Asikwambie mtu, Ilikuwa issue hasa. Wanaume waki herero na wake zao wakitumikishwa kwenye mashamba ya wajerumani. Tena kwa kulipa ujira wa mwira… ujira mdogo sana. Halafu kwa mbinde. Walinyang’anywa mashamba yao yenye rutuba na wajerumani wakajitwalia yawe yao.iliumiza sana.

Kana kwamba hiyo haitoshi wajerumani wakanza hata kutembea na mabinti na wake walio kuwa warembo waki bantu. (Imagine hapa jinsi gani unazidi kumwuudhi mwafrika) Wanaume waliumia sana kuona madhira yale yakifanyika katika jamii yao. Huku wakitizama tu.wakaona wasiwe wanaume suruali. Wajerumani walikazana kuwatumia watu wale kwa manufaa ya nchi yao ujerumani. Ardhi nzuri ilichukuliwa na wajerumani na kuwageuza waafrika vibarua kwa ujira mdogo sana. Kama vile haitoshi kuna reli ikajengwa kati kati ya kabila hili kuwagawa makundi mawili ili hiyo reli iende kwenye machimbo ya kopa huko Tsumeb na kuwanyang’anya sehemu kubwa ya ardhi hawa wazawa.

WANAUME WAKAJIPANGA KUONESHA URIJALI WAO.

Chifu Samuel Maharero aliamua sasa inatosha ...Kama mbwai mbwai.ama zao ama zetu.akakusanya vijana na watu wengine wenye uwezo, na kuwapa maneno yenye morali kwa ajili ya kwenda kupigania nchi yao. Aliwaambia kabisa kwa jinsi alivyokuwa muungwana. Hakuna kuua wanawake, hakuna kuua wamishionari, hakuna kuua watoto, hakuna kuua wazungu ambao si wajerumani au kabila lolote lile mbali na ujerumani. Alitaka wakapigane wao wa deal na wanajeshi,wanaume na viongozi waliokuwa wakisababisha mateso yenye chuki kwenye ardhi au nchi yao.
1200px-SamuelMaharero.jpg

Kapten wetu huyu sis wabantu Samuel Maharero mcheck alivyoweka pozi akiwaza namna ya kuwakomesha Wajerumani.

Wakifanya haya maandalizi walikuwa makini habari zisiwafikie wajerumani maana walitaka kuwashtukiza. Basi waherero wakafuata maagizo ya kiongozi wao walivamia mashamba ya wale wazungu na kuanza kuwaua. Walipoua wanaume waliwachukua wanawake na watoto na kuwasindikiza kurudi majumbani kwao. Hawakutaka kuua wanawake wala watoto. Habari zikasambaa kwa wajerumani wengine… lakini mpaka hapa waherero walikuwa wamefanikiwa kurudisha sehemu kubwa ya mashamba yao ukiacha kwenye ngome ya wajerumani. Huku kukawa kuna ugumu mkubwa sana

Wakoloni wakaanza kujiongeza kwa kuomba msaada wa kijeshi toka maeneo mengine chini ya kamanda Lothar Von Trotha aliyekuwa katili kama Goliath. Huyu alikuwa tayari ameshajikumbia sifa nyingi sana za ku deal na machafuko kama haya .. yaani kwenye CV yake kama ungesoma ungefaham huyu jamaa alikuwa ni mtu gani. kwanza alikuwa China huko kipindi cha nyuma na alizima machafuko kama haya mwaka 1901 dhidi ya wa Ihetuan na kabla ya hapo pia alisha fanya kazi kama hiyo huko East Afrika Tanganyika kwa kabila flan lililokuwa likifahamika kama wahehe. So jamaa huyu alikuwa na CV imeshiba hasa. Alikuwa katili ile mbaya…hakuwa mtu wa kufanya naye masikhara maana dakika chache tu damu ingemwagika.na hapa damu si yake..no. ya kwako ingemwagika ndani ya dakika chache sana.

Yeye alikuwa akiamini kuwa Makabila ya kiafrika huwa yanaelewa kupitia umwagaji wa damu tu hakuna namna nyingine.(yaani kusikia kwa kenge mpaka atoke damu masikioni) Masuala ya kujadiliana na kuwekekeana mikataba kwake ilikuwa ni upuuzi. Kwamba kwa waafrika ni kuwapa tu ngumi jiwe hapo ndo akili zao zinakaa sawa. Akasema “nitayaangamiza makabila ya kiafrika kwa pesa na mafuriko ya pesa na damu na ni katika hili ndipo jamii za kiafrika huelewa na mwishowe kuwafanya wajerumani waishi kwa Amani. Hili lijamaa lilikuwa liovu sana.

Basi ilipofika Agost 11 1904 wahereo (ovaherero) walijikusanya wote sehemu moja inaitwa Ohamakari (wateberg) walikuwepo wanawake na watoto wakiwa na mifugo yao. Baada ya kuwa kumetokea mapambano ya kivita wao wakawa wamekusanyika hapa wasijue la kufanya wakati huo wanaume wakiendele kuchapana na wajerumani. Kule wajerumani wakitumia silaha za kisasa walifanikiwa kuwashinda wanajeshi wa herero. Hivyo wakawafuata mapaka huku waliko wanawake, watoto na wazee ambao walishaamua kuondoka kukimbia makazi baada ya kuona hali si shwali kwa upande wao.

Wanajeshi wa kijerumani waliamua kuwafuata huku maskini hawa wasiojiweza.Walikuwa wakiwafuata kuwasukumia jangwani wakati huo huo kila chanzo cha maji huko njiani walikuwa wamekimwagia sumu. Baada ya kama week saba hivi zilizofuta Oktoba 2 mwaka huo huo Trotha aliwatangazia askari zake wa kishetani kama yeye kuwa sasa wawaswage ndugu zetu wale kuelekea Jangwani. Ili wakafie huko wote. Wakielekea katka kutimiza hilo kusudio la kishetani kabisa waliendelea kuua kila mherero waliyekutana naye.awe ameshika bunduki au hajashika.awe mtoto au mkubwa.ilikuwa ni kumimina tu risasi. Mpaka kwa mifugo. Ilikuwa issue hasa kwa wanamibia wale maskini.

Trotha pia aliwaambia kwa wale ambao watakuwa wamejisalimisha basi waendelee kupiga risasi usawa wa vichwa vyao ili wakimbie kuelekea kwenye jangwa huko Omaheke wakafe kwa mateso kwa kukosa maji,kuchoka na jua kali.hapa wajerumani hawa walikusudia kabisa kuonesha jinsi gani wana deal na waasi kikatili ili liwe funzo kwa wengine.ilikuwa ni kuwaonesha “cha mtema kuni hasa” haya yalikuwa ni mauaji ya Halaiki kulingana na tamko la UN kuwashughulikia wahalifu wa Mauaji ya halaiki mwaka 1948. Inasemekana Zaidi ya waherero 100,000 waliuawa kinyama katika tukio Hilo. Na wengine kama 20,000 waliachwa na vilema.

NAMA NAO WAAMUA KUVUNJA MAYAI VIZA

Mwaka huo huo 1904 kabila la Nama wakiongozwa na kapten Hendrik Witbooi (ngumi jiwe) nao waliamua kuasi na kupambana na wajerumani upande wa kusini mwa Namibia. Hawa wa Nama waliposhuhudia kilichowapata ndugu zao wa Herero hakuwakukatishwa tama badala yake hasira iliwaka ndani yao nao waka asi pia. Hawa waliepuka kupigana mapigano ya wengi. Walikuja na mbinu ya kupigana wachache wachache kwa makundi. Waliwasumbua sana wajerumani.

Kapten Hendrik Wibooi wa Nama.jpg

Kapten Hendrik Wiboo
Maskini kutokana na uduni wa silaha zao nao walikutwa na dhahma kama iliyowakuta ndugu zao wa herero. Waliomba wasitishe mapigano na kuwa yasitokee yale yaliyotokea kwa ndugu zao wa herero. Wajerumani waliwakubalia wakiwaahidi kuwa watasitisha vita na kila kitu kitakuwa shwali. Kinyume na makubaliano hayo wajerumani wakawachukua hawa Nama na kuwafanya wafungwa.walichukuliwa wanawake, watoto, wanaume na wazee na kuwekwa kwenye kambi za mateso wakichanganywa na waherero ambao walikuwa wamegoma kufa kule mwanzoni. Wengi wakafa kwa utapiamlo, mazingira magumu, njaa na magonjwa. Wengine wakatumika kama watenda kazi katika shughuli mbali mbali za kiuchumi katika mazingira magumu sana nao wakafa huko utumwani. Maskini inasadikika waliuawa wa Nama Zaidi ya 10,000.

ADUI MKUU WA BINADAMU SI MNYAMA ASIKUDANGANYE MTU

Matukio haya ya kutisha ya binadamu dhidi ya binadamu wenzie ni moja ya mambo yanayosikitisha kuwa anayeua binadamu kwa asilimia kubwa ni binadamu mwenzie na si wanyama. Mafuvu ya mashujaa wa kiherero yalichukuliwa na kupelekwa berlin huko ujeruman yakiwa yamewekwa kwenye masanduku ili kwenda kutoa ushuhuda jinsi gani wajeruman walivyo na nguvu hapa duniani na kumbukumbu pia kwa isku zijazo.

MIAKA KADHAA BAADAYE

Mwaka 2011 waliteuliwa wanamibia kadhaa ambao walienda Berlin kuchukua mabaki ya mafuvu ya wazaz na babu zao kama ambavyo walisimuliwa kuhusiana na vita ile na mafuvu kuchukuliwa kupelekwa ujeruman. Ilikuwa huzuni kuu kwa wanamibia hawa. Kushika mafuvu ya jamaa zao waliouawa kwa maumivu makali na mateso yaso kifani.

Na ukirudi nyuma Mwaka 1985 taarifa ya Whitaker ilisema wazi kuw alile tukio lilikuwa na nia ovu ya kuwafutilia mbali wanajamii wa kabila la hereoro na nama kusini magharibi mwa afrika hivyo kuwa Ni mauaji ya kwanza kwanza ya aina halaiki kwa karne ya 20.

Mwaka 1998 rasi Roman Herzog wa Ujeruman alitembelea Viongozi wa kiherero na alifanikiwa kuona na Chifu Munjuku Nguvauva ambaye yeye alitaka wajerumani waombe radhi kwa umma na pia walipwe. Herzog alimjibu chifu kuwa sharia ya kufanya malipo kwa makosa miaka hiyo haikuwepo mpaka mwaka 1907 so wasingeweza kuwalipa. Waherero wakafungua kesi huko Marekani mwaka 2001 wakitaka walipwe na bank ya Ujeruman ambayo ndiyo iliyokuw aikiwafadhiri hawa watawala wa kijerumani miaka hiyo wanawaua waafrika wenzetu kama panya..
index.jpg

Mwaka 2017… mwezi wa kwanza tena huko waliokuwa ndugu wa waathirka wa vita vile kwa makabila ya herero na nama walifungua tena kesi nyingine ya madai. Madai yao hayakusema ni kiwango gani walitaka walipwe kutokana na kufanyiwa unyama na ukatili wa kiwango cha juu.



MWISHOWE.

Agusti 2008 Peter katjavivi aliyekuwa balozi wa Namibia nchini Ujerumani alitaka mafuvu ya watu wa herero na nama yaliyochukuliwa mwaka 1904-08 yarudishwe na yaje kuzikwa Namibia kwa heshima …maana walikuwa makamanda hawa. Wapambanaji dhidi ya udhalimu wa mtu mweupe katika ardhi yetu ya afrika ambayo tulizawadia na Baba Mungu kwa mapenzi makubwa sana kwetu. Na hatimaye Septemba 2011 yakarudishwa mafuvu ya mashujaa wetu wa kibantu waliokuwa wamejitoa kupambana na wajerumani makatili yakiongozwa na Trotha. Mtu mbaya sana huyu jamaa.

14021001.jpg
bqQYDHW.jpg
 
hlf bado tunaendelea kuwaamini wazungu! dhima yao yakuitawala afrika bado inaendelea kwamaana wanataka mali.
tunajua kabisa kuna ukoloni mamboleo lkn kujiepushanao tunaona kama kazi ya kusaga meno!
bado muafrika hajaeshimika na kadri tunavyodhidi kuwakubalia ndo wanazidi kutubana.. Ukitaka kujua upuuzi ni ktk maswala ya imani Mungu waliekujanae kutuhubiria wenyewe hawakumuogopa!! ati usiuwe! kwahiyo wenyewe walikuwa wanasinzisha watu..?
ubatili mtupu huu!
tumekuwa na historia mbaya toka walivyokuja hawa viumbe vita,utumwa,unyonyaji sahivi wameleta ushoga na usagaji! nafikiri tunahitaji upembuzi ktk kufuata vitu vya hawa jamaa.
 
hlf bado tunaendelea kuwaamini wazungu! dhima yao yakuitawala afrika bado inaendelea kwamaana wanataka mali.
tunajua kabisa kuna ukoloni mamboleo lkn kujiepushanao tunaona kama kazi ya kusaga meno!
bado muafrika hajaeshimika na kadri tunavyodhidi kuwakubalia ndo wanazidi kutubana.. Ukitaka kujua upuuzi ni ktk maswala ya imani Mungu waliekujanae kutuhubiria wenyewe hawakumuogopa!! ati usiuwe! kwahiyo wenyewe walikuwa wanasinzisha watu..?
ubatili mtupu huu!
tumekuwa na historia mbaya toka walivyokuja hawa viumbe vita,utumwa,unyonyaji sahivi wameleta ushoga na usagaji! nafikiri tunahitaji upembuzi ktk kufuata vitu vya hawa jamaa.
Kweli hawa watu ni washenzi sana hawahitajiki. Lakini pia mageni yoyote kutoka nje ya Afrika ni majizi na mauaji maana hata miarabu haifai, ichukiwe sana. Ni majizi na mauaji hayo futilia mbali.
 
Nimejikuta nikiwa ktk hali ya majonzi sana, arafu MUNGU yupo anaangalia yoye haya, hivi sisi waafrica tulimkosea nini Mungu[emoji31][emoji31]
 
hlf bado tunaendelea kuwaamini wazungu! dhima yao yakuitawala afrika bado inaendelea kwamaana wanataka mali.
tunajua kabisa kuna ukoloni mamboleo lkn kujiepushanao tunaona kama kazi ya kusaga meno!
bado muafrika hajaeshimika na kadri tunavyodhidi kuwakubalia ndo wanazidi kutubana.. Ukitaka kujua upuuzi ni ktk maswala ya imani Mungu waliekujanae kutuhubiria wenyewe hawakumuogopa!! ati usiuwe! kwahiyo wenyewe walikuwa wanasinzisha watu..?
ubatili mtupu huu!
tumekuwa na historia mbaya toka walivyokuja hawa viumbe vita,utumwa,unyonyaji sahivi wameleta ushoga na usagaji! nafikiri tunahitaji upembuzi ktk kufuata vitu vya hawa jamaa.
Sizani kama ntaendelea kunyoosha kongoro zangu kwenda kanisani, hiyo ratiba ya kusali ndio imeshatoka sizani kama itajirudia tena. wadhungu kuku sana
 
Kweli hawa watu ni washenzi sana hawahitajiki. Lakini pia mageni yoyote kutoka nje ya Afrika ni majizi na mauaji maana hata miarabu haifai, ichukiwe sana. Ni majizi na mauaji hayo futilia mbali.
kabisa
 
Hakuna anayepata hasara. Wewe kuwa huru na maamuzi yako huna haja ya kuhangaika hangaika

Sizani kama ntaendelea kunyoosha kongoro zangu kwenda kanisani, hiyo ratiba ya kusali ndio imeshatoka sizani kama itajirudia tena. wadhungu kuku sana
 
sasa hapo wanamibia wa kipindi hiki wanataka walipwe kwa kuteseka kupi?

yaani wazee wateseke zaidi ya miaka 100 iliyopita wewe kiningina udai fidia dah
 
Back
Top Bottom