Michael 007
New Member
- Aug 11, 2022
- 1
- 0
UTANGULIZI.
Tupo katika zama za utandawazi; Sayansi na teknolojia imechukua nafasi kubwa Sana katika ulimwengu huu wa Sasa hususan katika shughuli mbalimbali za uzalishaji wa kiuchumi, mambo ya siasa, elimu, pamoja na masuala ya kijamii.
Teknolojia
NI ujuzi wa kutumia vyombo (mashine) Ili kurahisisha Kazi. Kupitia teknolojia tunaweza kubadili historia ya maisha yetu kiuchumi, kielimu,kijamii na kuwa tofauti na Ilivyokuwa hapo awali, pia tunaweza kubadili malighafi kuwa bidhaa yenye thamani kubwa na kukidhi mahitaji ya binadamu.
Teknolojia na kilimo.
Idadi kubwa ya watanzania wanaishi Kwa kutegemea kilimo.teknolojia ikitumika ipasavyo katika upande huu itachochea mageuzi makubwa Sana ya kiuchumi Kwa mtu mmoja mmoja pamoja na taifa kwa ujumla.
teknolojia itumike ipasavyo kufanya tafiti mbalimbali za kisayansi kuhusu mazao yatokanayo na kilimo Ili kuchochea uzalishaji mkubwa wa mazao mbalimbali na kuwa na kilimo Cha uhakika na chenye tija.
Teknolojia na uchumi.
Ili kufanikiwa katika shughuli mbalimbali za uzalishaji wa bidhaa na huduma na kutosheleza mahitaji ya Kila siku, katika zama hizi za utandawazi ni muhimu kujibidiisha katika shughuli mbalimbali za uzalishaji wa kiuchumi zinazofanyika Kwa njia ya kidijitali, hivyo ni vyema kutumia ipasavyo teknolojia Ili iweze kuleta manufaa yanayohitajika. Asilimia kubwa ya watu pamoja na makampuni mbalimbali wameweza kutajirika kupitia teknolojia, hivyo basi sekta hii ya teknolojia inapaswa kuangaliwa Kwa jicho LA tofauti.
Teknolojia na elimu.
Katika zama hizi za utandawazi elimu na teknolojia zinapaswa kwenda Kwa pamoja. Tukiwekeza maarifa na ujuzi wa kutumia Teknolojia tunaweza kubadili historia ya mtu mmoja mmoja pamoja na taifa kwa ujumla kuwa tofauti na Ilivyokuwa hapo awali. Kwa vijana ambao wapo mashuleni huu ni muda wa kuchangamkia fursa kuhakikisha wanapata maarifa yakutosha pamoja na uelewa juu ya umuhimu wa Teknolojia pamoja na matumizi yake katika nyanja mbalimbali Ili kuleta utatuzi wa matatizo na changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika jamii zetu na taifa kwa ujumla.
USHAURI.
Napenda kuihimiza serikali, jamii, taasisi mbalimbali pamoja na mtu mmoja mmoja kutumia teknolojia ipasavyo Ili kuleta manufaa yanayohitajika katika upande wa kiuchumi,elimu kilimo Ili iweze kuleta tija inayohitajika pamoja na maendeleo.

Upvote
1