Mtogweche
New Member
- Jul 2, 2023
- 3
- 1
Tupate maana fupi ya maneno haya katika kiswahili.
Kama ilivyonukuliwa kutoka kwenye kamusi ya kiswahili ya TUKI maneno haya yana maana ifuatayo.
SAYANSI ni mchakato wa kisomi wa kugundua na kuchunguza kanuni na sheria za asili zinazoelezea ulimwengu tunaoishi.
TEKNOLOJIA ni bidhaa,mbinu, na taratibu za kiufundi zinazotumika katika ujenzi wa vitu na vifaa vya kiufundi au katika utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo.
Teknolojia ni kitu ambacho kina uhusisha nyanja nyingi kama vile habari,mawasiliano na ujenzi.
Katika dunia ya leo,SAYANSI na TEKNOLOJIA ni vitu ambavyo vinaangaliwa zaidi kwenye upande wa maendeleo ya nchi hasa katika nyanja ya kiuchumi na uwezo wa kijeshi kama ilivyo katika nchi za Marekani,China na Urusi.
Dhana iliyojificha,Teknolojia na Sayansi imesaidia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya kisiasa na utawala bora.
Inastusha ni kivipi?
Majibu ya swali hili ni mfano hilisi.
Matumizi ya mfumo wa kimtandao katika kupiga kura unalenga kuimarisha utendaji wa haki katika uchaguzi.Nchi kama Kenya na Marekani zinatumia mifumo ya kimtandao katika chaguzi zao.
Hebu tuangalia kiundani jinsi Sayansi na Teknolojia zinaweza kuimarisha uwajibikaji na utawala bora katika nyanja mbalimbali.
ELIMU
Teknolojia imekuwa ikipigiwa debe katika kuhakikisha ufanisi wa ufundishaji unaongezeka.
Endapo tutamia mifumo sahihi katika kuhakikisha walengwa(walimu na wanafunzi) wanatimiza wajibu wao.
Mifumo ya kisasa inaweza kutumika katika kuhakisha walimu wanahudhuria kazini.Sio hivyo tu,pia kutimiza wajibu wa kufundisha.
Teknolojia ya kamera inaweza kutumika katika kuangalia kama mwalimu ametimiza wajibu wake.Pia,inasaidia katika kutathimini ufundishaji wake.Kusaidia,kuzuia vitendo vya kikatili zinavyofanywa na baadhi ya walimu wasio wawajibikaji.
Je,wanafunzi hawana wajibu?
Wajibu wa wanafunzi ni kuhakikisha ana hudhuria shule na kupata elimu.
Kwenye kufanikisha hilo,uhifadhi wa taarifa za wanafunzi kwa njia ya kisasa itawezesha ufuatiliaji makini na usahihi zaidi,na kuhakikisha wanawajibika ipasavyo.
HAKI ZA BINADAMU
Haki za BINADAMU ni moja ya vitu ambavyo zinaenelezea moja kwa moja uwepo wa uwajibikaji na utawala bora katika taifa.Kuvunjwa kwa haki za binadamu kunaonesha kuwa hakuna uwajibikaji na utawala bora.
Sayansi na Teknolojia inahusika kwa namna gani?
Maendeleo ya Teknolojia yamesaidia kwa kiasi kikubwa katika kupigania haki za binadamu.Mitandao ya kijamii imekuwa ikitumika kutoa elimu juu ya haki za binadamu.Maendeleo hayo yamechangikia kwa kiasi kikubwa katika kufichua vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamukatika jamii.
Matukio mbalimbali ya uvunjifu wa haki za binadamu yamekuwa yakionekana kwenye vyombo vya habari na kupingwa vikali.
Katika tukio la hivi karibuni ambalo limezua taharuki nchini ufaransa baada ya askari kufanya mauji ya kijana mwenye umri wa miaka 17 kwa kutumia risasi.Teknojia ya habari imehusika kwa kiasi kikubwa na kuhakikisha suala hili ambalo linahusishwa uvunjifu wa haki za binadamu linapingwa.
Chanzo: DW
UKUSANYAJI MAPATO
Hili ni suala ambalo linahitaji uwajibikaji wa hali ya juu kwani inahusisha fedha.Kutokana kuimarika kwa uwajibikaji,miaka ya hivi karibu makusanyo ya mapato yameongezeka kwa kiasi kikubwa.
Je,unafiri ni nini kimechangia uwajibikaji huo?
Jibu ni TEKNOLOJIA
Teknolojia imesaidiaje?
Teknolojia imechangia Kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha uwajibikaji katika ukusanyaji mapato.Matumizi ya mtandao katika kufanya malipo yamesaidia katika kupunguza ubadhilifu wa fedha za umma.
Tupe mfano halisi?
Matumizi ya mifumo ya kisasa kwenye ukusanyaji mapato kama vile ushuru kwa kutumia mashine za EFD kumeimarisha kwa kiasi kikubwa uwajibikaji na kupunguza ubadhilifu.Hivyo,kuongeza ukusanyaji mapato.
Sio hivyo hata,kuwepo kwa mawasiliano ya kutoa taarifa za rushwa kumefanya kuongeza kwa uwajibikaji wa watendaji katika sekta hii.
MALEZI
Wazazi na jamii kwa ujumla wana wajibu mkubwa ya kuhakikisha wanawapa watoto malezi sitahiki ili kuhifadhi hadhina ya kutegemewa katika taifa.Japokuwa ,baadhi ya wazazi hawatambui kiundani juu ya wajibu wao kwenye malezi ya watoto.Baadhi yao, wamekuwa wakipuuzia wajibu wao katika malezi ya watoto.
Je Teknolojia inasaidia namna gani?
Teknolojia ni muhmu katika kuhakikisha wazazi ambao hawatambui wajibu wao wana elimishwa.Hii imekuwa inaweza ikafanyika kutumia televisheni na redio.
Kupitia teknolojia ya habari,imetoa nasaada mkubwa sana katika kufichua wazazi ambao wanapuuzia wajibu wa kulea watoto ipasavyo na kutaka kuwakosesha haki zao za msingi kama elimu.
Tukio la hivi karibuni limeripotiwa habari kuhusu Wazazi ambao walitaka kumuozesha msichana ambae amefaulu na anabidi aendelee na masomo.
Chanzo:Millardayo
Teknolojia ya mawasiliano bila shaka imehusika moja kwa moja katika kutoa taarifa juu ya jambo hili kwa mamlaka husika.PiaTeknolojia ya habari imehusika katika kutoa taarifa ya jambo hili na kuelimsha jamii kuwa suala hilo halifai.
HITIMISHO
Maendeleo ya SAYANSI na TEKNOLOJIA ni kitu ambacho kinabidi kutazamwa kwa ukaribu sana,kwani ni muhimu sio kwenye maendeleo ya kiuchumi tu pia katika kuimarisha uwajibikaji na utawala Bora.
Hivyo,Serikali kwa kushirikiana na wadau na wawekezaji katika Teknolojia wanawajibu katika kuweka mikakati madhubuti katika maendeleo ya SAYANSI na TEKNOLOJIA kwani kufanya hivyo tutakuwa tumepiga ndege wawili kw
a jiwe moja kama waswahili wanavyosema.

Upvote
1