Aidarus Ally
Member
- Aug 18, 2022
- 8
- 7
UTANGULIZI
Sayansi na teknolojia ni maneno mawili tofauti lakini yana maana zinazohusiana, Sayansi ni elimu inayoambata na majaribio kuhusu kitu fulani lakini teknolojia ni matumizi ya sayansi ambayo hutumika kutengeneza vifaa vitakavyotumika kutatua mambo,kwa maana hiyo kuna uhusiano mkubwa baina ya maneno haya mawili.
SAYANSI NA TEKNOLOJIA WAKATI WA ZAMANI HAPA TANZANIA
Hapo mwanzo nchini Tanzania hapakuwa na athari ya ukuaji wa sayansi na teknolojia,kbwani kulikuwa na teknolojia duni sana hata hivyo njia za asili ndizo zilizotumika sana, Mfano hapakuwa vyombo vya habari ambavyo vingerahisisha upatikanaji wa habari, vilevile hapakuwa na vifaa vya kisasa kwa ajili ya kilimo, pia kulikuwa na changamoto ya viwanda vya kisasa, yote haya yamepelekewa na kutokuwa na teknolojia nzuri.
SAYANSI NA TEKNOLOJIA WAKATI WA SASA TANZANIA
Kwa wakati huu nchini Tanzania kumekuwa na ukuaji wa sayansi na teknolojia kwa kiasi ukilinganisha na hapo zamani, mfano sasa hivi kuna Vituo vingi vya redio(clouds fm,Sibuka fm, redio one,redio free africa)vituo vya runinga kama(TBC taifa,AZAM tv,itv)magazeti(Nipashe, Mwananchi,Raia mwema) majarida,makala na vitabu na vyombo vinginevyo,hata pia uwepo mwingi wa viwanda hususani jijini dar es salaam.
ATHARI YA UKUAJI WA SAYANSI NA TEKNOLOJIA KWA SEKTA MBALIMBALI NCHINI TANZANIA
Sekta ya biashara; sekta hii imeathiriwa zaidi na Ukuaji wa sayansi na teknolojia kwa hivi sasa nchini Tanzania, kupelekea kujengwa kwa benki mbalimbali kama Crdb,Nmb,Nbc,Amana benki,kcb, diamond trust,Akiba benki na nyinginezo na kupelekea wafanyabishara kuwekeza pesa nyingi katika biashara na kufanya malipo ya aina yoyote kwa haraka zaidi tofauti na hapo zamani yote hii inachangiwa na ukuaji wa sayansi na teknolojia, kufanyika kwa biashara za kimtandao kuwezesha bidhaa kujulikanwa na wateja wengi kwa muda mfupi sana,kwa uchache huo ndio mchango wa sayansi na teknolojia katika sekta ya biashara.
Sekta ya elimu; nchini Tanzania sekta hii inaendelea kukua zaidi tofauti na hapo zamani kutokana na mchango wa ukuaji wa sayansi na teknolojia, mchango huo ikiwemo kuweza kudahili maelfu ya wanafunzi kwa muda mfupi,kupanga takwimu zinazohusu elimu kupitia kompyuta na kuhifadhi kumbukumbu zinazohusu elimu nchini,hivyo kuweza kutambua uhitaji wa walimu kwa kuangalia takwimu zilizopo,hivyo sayansi na teknolojia ina umuhimu mkubwa sana katika sekta ya elimu,kwa kuliona hilo sekta ya elimu imeweka mkazo zaidi katika masomo ya sayansi.
Sekta ya usafirishaji; kwa sasa nchini Tanzania kuna vyombo vingi vya usafirishaji ukilinganisha na zamani uwepo wa ujenzi wa miundombinu mbalimbali kama barabara na reli mfano kwa upande wa usafiri wa nchi kavu ni magari,treni usafiri wa majini ni meli,maboti usafiri wa angani ni ndege, uwepo wa vyombo hivi umechangiwa zaidi na ukuaji wa sayansi na teknolojia hivyo kupelekea usafirishaji kuwa ni wa urahisi na kuwezesha usafirishaji wa mizigo mizito na mingineyo.
Sekta ya kilimo; Hapo mwanzo mfano wa nchi kama Tanzania katika suala la kilimo wakulima walikuwa wakitumia njia duni za kilimo kwa kulikuwa na vifaa duni hivyo kupelekea kulima maeneo madogo kwa kutumia nguvu kazi kubwa,lakini kwa sasa wakulima wengi nchini Tanzania wanatumia njia za kisasa mfano matumizi ya mbolea za kisasa kama npk katika kuhakikisha yanapatikana mazao bora,matumizi ya trekta katika kuandaa mashamba makubwa hivyo kupelekea kupatikana kwa mazao mengi na matumizi ya madawa ya kuulia wadudu ambayo yanasaidia kuzuia mazao yasiharibiwe na wadudu,njia zote hizi zinapatikana kwa kuchagizwa na ukuaji wa sayansi na teknolojia.
Sekta ya afya; Uwepo wa ukuaji wa sayansi na teknolojia umeweza kurahisha namna ya utoaji huduma na upatikanaji wa vifaa tiba ambavyo vinatumiwa hospitalini mfano hapa Tanzania kuna hospitali nyingi za kiserikali na binafsi mfano hospitali ya muhimbili kuna vifaa vya kufanyia opereseheni za kisasa,vifaa vya kukagua mwili mzima,x-ray na hadubini za kutosha ambavyo vinarahisisha namna ya kuwahudumia wagonjwa,pia huraahisisha upatikani wa madawa mbalimbali.
Sekta ya habari na mawasiliano; katika sekta zote ,sekta ambayo ina athariwa zaidi na ukuaji wa sayansi na teknolojia ni sekta ya habari na mawasiliano hapa Tanzania,uwepo wa vifaa vya mawasiliano kama rununu,runinga, kompyuta na vinginevyo vimerahisha mno upatikanaji wa habari,lakini vifaa hivi visingekuwepo pasi na uwepo wa sayansi na teknolojia ambavyo vyombo hivi vyote watu huvitumia kupashana habari kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa haraka zaidi nchni Tanzania.
SAYANSI NA TEKNOLOJIA KWA VIJANA WA SASA NCHNI TANZANIA
Nchini Tanzania kwa wakati wa sasa ukuaji wa sayansi na teknolojia unaathiri sana vijana iwapo kama watatumia vibaya hivyo sayansi na teknolojia na kupeleka mporomoko wa maadili kwa kupiga na kurekodi video za utupu na kutuma mitandaoni, lakini kwa ujumla ukuaji wa sayansi na teknolojia nchini Tanzania una umuhimu mkubwa sana kwa vijana kwani ni chanzo cha ajira,chanzo cha kupata mafunzo mbalimbali kupitia mitandao.
FAIDA ZA MATUMIZI SAHIHI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA KWA JAMII ZA KITANZANIA
(1) Kupata ajira
(2) Kujenga uhusiano mzuri kwa kuwasiliana na watu mbalimbali
(3) Kujifunza vitu tofauti tofauti kama mapishi,urembo kupitia mitandao
(4) Kuhifadhi taarifa mbalimbali kwenye vifaa kama kompyuta au simu
HITIMISHO; Lengo la kuichagua hii mada ni kuonesha namna gani sayansi na teknolojia ilivyo na umuhimu sana katika kila nyanja, Nyanja ya habari na mawasiliano,biashara,afya,elimu,kilimo na biashara,na lau sayansi na teknolojia ikizingatiwa katika matumizi sahihi basi itakuwa chachu zaidi katika maendeleo.

Upvote
2