SoC02 Sayansi na Teknolojia Tanzania

SoC02 Sayansi na Teknolojia Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

Jacksonmyula

New Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
3
Reaction score
2
SAYANSI NA TEKNOLOJIA TANZANIA
Katika nchi yetu ya Tanzania sayansi na teknolojia imekua chini sana na imekua vigumu katika kuboresha sayansi na teknolojia kwani nchi nyingi za afrika tupo nyuma katika suala zima la sayansi na teknolojia ila kwa upande wa Tanzania serikali imekua ikiboresha mara kwa mara miundo mbinu katika suala zima la sayansi na teknolojia lakini bado tumekuwa tupo nyuma kuna baadhi ya nchi ambazo wamepiga hatua kubwa katika hili suala la sayansi na teknologia na hawana serikali kama ya nchini kwetu nikimaanisha nchi yetu imejaa amani lakini bado nchi yetu ipo nyuma katika mambo mbalimbali. Kwa upande wangu naona serikali imeipa sana kipaumbele nyanja ya Afya kwenye suala zima la sayansi na teknolojia likini inatakiwa kuhakikisha nyanja zingine kama elimu nayo inapewa kipaumbele katika suala zima la sayansi na teknolojia.

NINI KIFANYIKE KUBORESHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA TANZANIA KWA WANAFUNZI?
Katika kuboresha sayansi na teknolojia serikali lazima iangazie katika elimu na watu binafsi kwani sayansi na teknolojia si kwa wanafunzi tu bali hata kwa watu binafsi ambao ni wabunifu.

Kwangu mimi naona iwapo serikali itafanikisha suala zima la sayansi na teknolojia kwa kiasi kikubwa hata uchumi wa nchi yetu unaweza kupanda kwa kupata wageni mbalimbali wanaokuja kuwekeza nchini ila katika hili suala kumekuwa na changamoto hasa kwa kuwa na wataalamu wachache wanao weza kusaidia uboreshaji wa sayansi na teknolojia ila kama serikali itaunga mkono suala la sayansi na teknolojia itakua rahisi kupata wataalamu mbalimbali katika nyanja mbalimbali hasa katika suala zima la afya. kwangu mim kama serikali itafanya yafuatayo itaweza kurahisisha ukuaji wa sayansi na teknolojia.

1. Serikali ingeweka utaratibu wakuchagua wanafunzi wenye ufaulu mkubwa walau hata mia moja (100) kila mwaka na kuwasomesha nje ya nchi ili kuweza kupata ataalamu walio bobea katika nyanja mbalimbali hasa ya utabibu hii itasaidia kwa miaka ya badae kuwa na watabibu wengi wenye taaluma kubwa. Lakini kwa sasa asilimia kubwa ya wasomi wanao soma nje ya nchi wanasoma kwa juhudi zao wenyewe nakupelekea wengi wao kuajiriwa nje ya nchi lakini kama serikali ikiamua kuwaandaa wanafunzi walau 100 kila mwaka watakao someshwa nje ya nchi hii itasaidia kuzalisha wataalamu wengi wenye ujuzi wa hali ya juu na baadae kuweza kupata wataalamu wengi nchini ambao watasaidia kuzaliza wataalamu wengine.

2. Serikali iweze kutoa motisha katika suala la sayansi na teknolojia kwa kuweka mashindano ya ubunifu ya kisayansi na teknolojia na kuweza kutoa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi watakao fanya vizuri katika sauala zima la ubunifu wa sayansi na teknolojia ikiwa ni pamoja na ajira kwa watakao fanya vizuri hii itasaidia sana katika suala zima la kuzalisha watu wenye teknolojia kwani itaongeza ushindani kwa wanafunzi wengi na pia itasaidia kuzalisha mifumo mbali mbali yenye ubora wa juu kwani kila mwanafunzi atakae ingia katika mashindano hayo atafanya kwa bidii kutengeneza mifumo yenye ubora ili waweze kushinda.

3. Serikali isaidie katika kuongeza vifaa vya kisasa zaidi vinavyoweza kutumika katika kukuza sayansi na teknolojia katika janja ya elimu hii itasaidia kukuza uelewa wa wanafunzi kwa kiasi kikubwa kwani wataweza kujifunza kwa vitendo zaidi. Katika suala zima la sayansi na tec]knolojia vitendo vinahitajika na sii elimu ya mdomo na maandishi kama serikali itaboresha miundombinu ya sayansi na teknolojia itasaidia katika kukuza taaluma ya wanafunzi kwa vitendo zaidi.


NINI KIFANYIKE KUBORESHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA TANZANIA KWA WATU BINAFSI?

Kuna baadhi ya watu binafsi wamejiajiri na wengine hawajajiari ila wana ubunifu wa kufanya mambo makubwa tena yenye kuleta tija katika suala zima la sayansi na teknolojia lakini mara nyingi hukatishwa tamaa tena na serikali yetu na wengine wanaacha mambo wanayo yafanya kuna baadhi ya wananchi wenye uwezo wa kutenegeneza vifaa mbalimbali vya kurahisisha kazi wengine wanauwezo wakutengeneza vifaa vinavyo zalisha umeme lakini hawanufaiki na serikali yetu. Kwa upande wangu kama serikali ikitoa misaada kwa wabunifu hawa hii itasaidia kukuza viwanda vidogo vidogo na itawasaidia wengi kujiajiri katika viwanda vyao.

Lakin serikali yetu imefumbia macho watu binafsi wenye ujuzi mbalimbali hivyo wengi wao huishia kukata tamaa kwa maan hawaoni mchango wa serikali yao.

PENDEKEZO
katika michezo kuna suala zima la umiseta kwa pendekezo langu hapa naona ili kukuza sayansi na teknolojia kwa haraka kungekuwa na mashindano kama ya umiseta ila haya yawe ya sayansi na teknolojia hivyo basi kila mkoa uwe na timu au vikundi vya wabunifu ambavyo vitaingia kwenye mashindano kundi litakalo shinda linaingia kwenye mashindano ya kitaifa hvyo kila mkoa utatoa kundi lililoshinda arafu baada ya hapo makundi yote yaliyo shinda katika ngazi ya mkoa yenashindana kupata kundi washindi watano watakao fanya vizuri na zawadi kutolewa kwa hao washindi watano pia serikali ikifanya hivi itapata programu mbalimbali za kisayansi na kiteknolojia ambazo zinaweza kuwa mchango mkubwa katika kukuza nchi au uchumi kwa kuwa na viwanda vidogovidogo. Hii itachangia kwa kiasi kikubwa kukuza sayansi na teknolojia kwenye nyanja za uchumi hasa kwa wajasiriamali, Elimu kwa wanafunzi kwani wengi wataingia kwenye mashindano ya kufanya vitu vyenye ubora zaidi ili kuhakikisha wanapata ushindi, Katika nyanja ya viwanda wengi watahakikisha wana buni mashine zitakazo kuwa na ushindani hvyo kupata wabunifu wengi zaidi hii kwa miaka ya baadae itasaidia kuwa na watu wenye akili za kugundua vitu vingi vyenye maslahi kwa jamii.
 
Upvote 4
Sema maigizo ya Sayansi hivi unajua tuna-import mpaka simple furniture toka Uturuki?
 
Lakini mbona kuna mashindano ya "Innovations competition" ambayo watu mbalimbali wanaonesha vumbuzi zao......... anyway wazo zuri

Pita na kwangu "Vita ya vijana dhidi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia"
 
Back
Top Bottom