SoC01 Sayansi na Teknolojia

SoC01 Sayansi na Teknolojia

Stories of Change - 2021 Competition

Gift swai

New Member
Joined
Sep 18, 2021
Posts
1
Reaction score
1
Habari wanajamii forum wenzangu, leo tutaangalia sayansi na teknolojia na vijana katika kuleta tija katika taifa letu.

Karne hii tumeona vile mapinduzi ya Sayansi na Teknolojia yakizidi kuongezeka, na kadri siku zinavyozidi ndivyo vitu mbalimbali vinazidi gunduliwa.

Kati ya uvumbuzi mkubwa wa Sayansi na Teknolojia ni simu janja(smart phone) na mitandao ya kijamii ambayo imefanikiwa kutawala maisha ya watu wengi sana kwani zimefanikiwa kufanya dunia kuwa kijiji na kurahisisha mambo mengi sana na kusaidia katika upatikanaji wa taarifa mbalimbali ikiwemo biashara, sanaa, Afya, Michezo, siasa, elimu na kadhalika na wengi tunawashukuru wavumbuzi wetu katika hilo.

Simu hizi janja hutumika kusomea na kufundishia, wafanya biashara kuweka bidhaa zao mtandaoni ili kutafuta wateja na wateja kutafuta bidhaa mbalimbali, kutafuta maudhui na matukio ambayo yanaendelea duniani nk.

Lakini ukiacha faida ya Sayansi na Teknolojia hii ya simu janja kuna athari nyingi sana ambazo tumeona zikijitokeza kutokana na matumizi mabaya ya simu janja hizi haswa kwa vijana ambao ni taifa letu la kesho. Kwan wengi wao wameshindwa kuzitumia simu hizi kutatua mambo mbalimbali ikiwemo kutafuta fursa zilizopo kiganjani mwao kama biashara za mitandaoni ambapo inakuwa rahisi kutafuta wateja kupitia wafuasi walionao katika mitandao ya kijamii. Lakini badala ya kufanya hvyo wengi wao kwa kukadiria tu katika asilimia 100, asilimia 70 ya simu janja hizi wanazitumia vibaya.

Nikiangalia sana sana katika taifa langu la Tanzania kupitia simu hizi Mitandao ya kijamii imekuwa ikitumiwa na vijana wengi bila kuleta tija yoyote katika Taifa letu. Vijana wengi hutumia simu kutafutau udaku kuhusu watu maarufu, kubashiri matokeo ya michezo, kuangalia sinema, kutupia picha na video mitandaoni Ili kupata wafuasi wengi katika kurasa za instagram, facebook, Tiktok nk, na hata wengine kuthubutu kujikita katika kuangalia picha au video za ngono. Hayo yote husaidia sana kupoteza mda katika mitandao ya kijamii ambapo vijana hawafaidiki kabisa. Teknolojia hii imepelekea vijana wengi kupotea katika usingizi mzito na kutojua lini wataamka katika usingizi huo. Kutumia simu janja hizi ambazo zina mambo mengi sana ambayo yasipotumiwa vizuri basi vijana hufeli mashuleni na kwa wale wasiokuwa na kazi kuzidi kubweteka.

Sasa je tunawasaidiaje hawa vijana ambao ni taifa letu la kesho katika kuepukana na matumizi mabaya ya Sayansi na Teknolojia hii?

1. Tujue tu katika kizazi cha karne hii watoto kwa vijana wamekuwa wajanja na wadadisi sana kwahiyo ni jukumu la kila mzazi au mlezi, jamii na walimu mashuleni kuwaelimisha watoto na vijana hawa ili waweze jua simu janja si tu za udaku bali ni za kujisomea na kukuza kipato chako binafsi na cha taifa lako.

2. Kutokuwapa watoto walioumri chini ya miaka 15 simu janja au unapowapa basi kuweka uangalizi au usimamizi wa simu hiyo ili kuepukana na kukutana na maudhuhi yasiyo wahusu au yasiyo wafaa.

3. Mitandao ya jamii kuweka vizuizi katika kurasa mbalimbali kwa vijana wenye umri chini ya miaka 18 na kuwaekea maudhui yanayolandana na umri wao.

4. Kuandaa semina kwa ajili ya vijana ambao wamemaliza kidato cha nne na kuendelea, ambapo watafundishwa jinsi ya kutumia simu janja na mitandao ya kijamii kwa ufasaha zaidi ili kujikwamua katika nyanja mbalimbali za maisha. Na kwa wale ambao wapo chini ya kidato cha nne kuzidi kuelimishwa mashuleni jinsi ya kutumia simu janja katika masomo yao.

5. Na mwisho kabisa vijana wanabidi waamke wenyewe sasa nakutambua kua kuna fursa nyingi ambazo zipo mikononi mwao wenyewe, kwahiyo katika kutafuta fursa hizo wanabidi watumie sayansi na teknolojia hizi vizuri

Katika yote hayo vijana hawana budi kutambua kuwa vitu vingi vinazi kuvumbulia kupitia science na teknolojia mbalimbali, na uvumbuzi mara nyingi hutokana na shida au tatizo fulani basi kama ni hivyo wanabidi watambue jinsi ya kutumia simu janja na mitandao ya kijamii vizuri kwani imeturahisishia kuwafika watu wote dunia kwa dakika tu ambapo apo nyuma haikuwa rahisi kabsa kwani ilikuwa inachukua mda sana kujua mambo ya mikoa au nchi nyingine. Na kwa kumalizia niwakumbushe tu mda ni mali na unaweza ukaamua kuvumbua au kufanya chochote katika umri wowote kwahiyo basi wajitahidi kufumbua macho yao na kutumia Sayansi na Teknolojia kuleta tija.

Asanteni
 
Upvote 1
Back
Top Bottom