SoC02 Sayansi na Teknolojia

SoC02 Sayansi na Teknolojia

Stories of Change - 2022 Competition

piry Lasway

Member
Joined
Jul 13, 2021
Posts
6
Reaction score
2
Mataifa makubwa na ya kati tunayoyaona leo yaliwekeza kwenye Sayansi na teknolojia,ndipo yalipofikia apa tunapoyaona.Ili taifa letu la Tanzania kuweza kukua halina budi kuwekeza kwenye sayansi na teknolojia kwa kukuza na kuendeleza vipaji vya wabunifu wetu.

Katika taifa letu tumesikia wabunifu mbalimbali, wengine wameishia madara ya chini tu lakini Mwenyezi Mungu amewapa vipawa,ambavyo vingewezeshwa na kukuza vingekuwa tija kwa taifa letu kwa ujumla. Tumesikia kuhusu mzee aliyebuni chanzo kipya cha kufua umeme kwa kutumia nguvu za sumaku,kijana wa Kigoma kutengeneza kituo cha redio, mwingine aliyetengeneza helikopta na wengine wengi.

Sasa kama Serikali ingevikuza na kuendeleza vipaji hivi, wangekuwa na mchango mkubwa katika taifa letu.


MAMBO AMBAYO SERIKALI INAPASWA KUFANYA ILI KUKUZA VIPAJI;

(1) Serikali kuja na mkakati wa kukuza vipaji kuanzia shule za msingi mpaka vyuo vikuu,kupitia shule za msingi mpaka vyuo vikuu kuwe na mashindano ya vipaji, kupitia hayo mashindano watoto watakua na ari ya kuonyesha uwezo wake katika ubunifu.

Baada ya kuvijua, serikali na wadau wengine watavikuza na kuviendeleza,kwa njia hii ama kwa hakika tutapiga hatua katika sayansi na teknolojia.

(2) Serikali kuendeleza na kukuza vipaji vya waliopo mtaani ambao wana vipaji, mtaani wapo wengi ambao wana vipaji, sema hawana pa kuvionyesha na waliovionyesha wamekosa sapoti ya kuviendeleza,mwishowe vimekufa ama vimelala tuli.

(3) Pia wadau wengine kimaendeleo kama sekta ya habari inamchango wa kuvitafuta na kuvionyesha kwa jamii vipaji vilivyopo,hii itasaidia jamii na serikali kuviona na kuvikuza.

(4) Serikali kuwasomesha vijana wenye vipaji vya ubunifu na waliochagua masomo ya sayansi,ili kupata wataalamu wengi wa sayansi.

Na Priscus Lasway.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom