SoC02 Sayansi na teknolojia

SoC02 Sayansi na teknolojia

Stories of Change - 2022 Competition

Bhuriga

New Member
Joined
Aug 24, 2022
Posts
3
Reaction score
1
SAYANSI NA TEKNOLOJIA

UTANGULIZI
Sjui ni Mimi tu au Kuna wenzangu ambao pia hukerwa na baadhi ya tabia mtandaoni kutokana na matumizi mabaya ya mtandao.

kupitia maarfa ya Sayansi na Teknolojia tumeona Faida nyingi ambazo zimesaidia mtu mmoja mmoja au kundi la watu kuweza kunufaika na maarfa hayo ikiwemo katika swala Zima la Mawasilino ,Habari ,Biashara ,kazi ,Ajira ,Afya na Wakati ikiwa tu mtumiaji atatumia vizuri maarfa hayo.

MAELEZO
Ila kumekua na matumizi ya hovyo hasa kwenye mitandao Kuna vitu vingi vya kuona, kuskia na kusoma na vitu hivyo havichagui umri Wala rika upotoshaji ni mwingi Sana na waathirika wakubwa ni watoto na vijana ambao wengi wao wamekua bila malezi au uangalizi wa wazazi ambao wapo bize Sana kutafta pesa za kuhakikisha hao watoto wanapata mahtaji yao bila kujua mtoto ana makundi yapi, anatumia nini ,anajifunza nini au je anachojifunza anakhtaji kwa wakati huo,

- vile vitu vya upotoshaji anavyo vitazama, kusoma na kuskia mtoto au kijana na akili yake ikiwa bado katika kuchanganua mambo anajikuta anaingia katka msongo ambao si wa lazma, hofu, maswali mengi yasiyo na majibu, huyu kijana anaamua nini cha kumsaidia ambacho pia si msaada Bali ni kumuuangamiza kwa asilimia chache Sana aneza kutambua msaada sahihi, akitafta wazazi ili apate msaada wapo bize na kazi na anaishia kurud Tena mtandaoni na kuanza kua sugu kwa kuona anachokifanya ni sahihi na anafanya bila kuangalia hisia za watu anao waumiza kwa kujiaminisha kua walimtazama hawakufanya kitu sasa kazi ni kwao.

- Sawa ni Dunia ya utandawazi ambapo kila mtu yupo huru kufanya kile anacho taka na maarfa ni mengi Sana ambayo yanapelekea hata kutegemeana kunapungua kwahiyo inakua Kila mtu na mambo yake si vibaya swali ni je,hayo unayoyafanya Yana utu ndani yake au unafanya tu kwasababu una uwezo wa kufanya na upo katka ulimwengu wa uhuru na wenye maarfa ambayo yanakurahsishia kufanya unachokifanya.

- Tunaona udhalilishaji unaoendelea mitandaoni mpaka unajiuliza Kwan hawa watu wanaofanya hivi hawana wazazi ,hawana ndugu ,hisia je ,lakin ukichunguza kiundani zaidi unagundua shida ipo kwenye malezi, Athari za Sayansi na Teknolojia bila usimamizi kutoka kwa wazazi au walezi ,Japo baadhi wamelelewa vizuri tu lakini alichojifunza kutokana na maarfa aliyoyaona ,kuyasoma au kuyasikia Yana pelekea kiburi na misimamo ambayo si msaada katka jamamii .

- Hivyo basi ni vema pamoja na Sayansi na Teknolojia kuturahisishia mambo lakini katka swala la pesa bado tujitahid hata kwa aslimia 50% kutenga muda kama wazazi au walezi kujichunguza sisi wenyewe lakini kuwachunguza watoto au vijana wetu katika ukuaji wao ili Kupunguza Athari hizi za Sayansi na Teknolojia kwa vijana Bali kuwaonyeshe njia sahihi ya wao kuifata ili maarfa hayo ya Sayansi na Teknolojia ya wanufaishe wao na jamii kwa ujumla kwa kufanya yafuatayo ....

- Mzazi au mlezi chunguza kwa umakini haya yafuatayo kwa mtoto au kijana wako
• Mtoto au kijana ana umri gani?
• Anakaa au anabaki na nani nyumbani ,akitoka anakua wapi na Akina nani kwa ajili ya nini, na je anachokifanya huko nje kina manufaa gani kwake na hasara au madhara yake ni yapi?
• Hupendelea kujihusisha na vitu gani?
•Rafiki zake ni wapi?
•Ratiba zao zipo vipi yeye na rafki zake ?
•Wanafundishana nini?
•Tabia gani hatarishi anazo au zinamkabili kutokana na umri au mwenendo wa maisha yake
• anakula nini?
• anavaa nini ?
• page gani hupenda kuzifatilia mtandaoni?
• anasoma nini ?
- Msikilize hata Kama anachokizungumza unahisi kina kupotezea muda Ila jitahdi kumskiliza, jitahidi kumwelewa, ustumie hofu au ukali kumkanya ,muuulize kwa utaraatibu mweleze Faida au madhara ya anachokifanya, tafta namna ya kumsaidia kuelewa Kama utamuadhibu basi hakikisha anatambua kosa la yeye kuadhibiwa.

- Msaidie kujiamini na kujiona ni Bora na kuwaona wengne ni Bora pia.
  • Msaidie katka kuchagua kilicho sahihi.
  • Tenga muda wa kua na watoto au vijana wenu pamoja ili muwafaham vizuri vivyo hivyo kwa vijana au watoto.
  • Wafundishe utii na kutambua makosa wanapokosea na nini wafanye baada ya kukosea bila kujali kimo, Hali ya kiuchumi, mazingira au umri.
HITIMISHO
Sayansi na Teknolojia ipo kwa ajili ya kutusaidia kupitia maarfa yake kama tutajua matumizi mazuri ya maarfa hayo na si kupotosha au kuondoka Hali ya utu ndani yetu.
Naombeni kura zenu 🙏
 
Upvote 0
Back
Top Bottom