BROTHER OF BROTHERS
Senior Member
- Jun 30, 2013
- 113
- 159
Nawasalimu wote mliopo kwenye Mtandao huu wenye Uhuru wa kujieleza.
Nimechukua fursa hii kuja na Mada ya kuomba sayansi ya kilimo kurudishwa Mashuleni kuanzia elimu ya msingi Hadi Sekondari.
Somo la Sayansi KILIMO ninaamini Wengi wetu haswa kaka na dada zetu walilisoma ingawa kwa uchache ila kutokana na ukweli kwamba "Kilimo ndiyo uti wa Mgongo wa Taifa Hili basi Kuna haja ya wizara ya Elimu kurudisha Somo la kilimo katika mtaala wa Elimu.
Binafsi Mimi ni kijana mtanzania msomi wa Shahada ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano "IT". Kutoka chuo kimoja kikuu hapa nchini kwetu.
Ni mwaka wa Tano mpaka sasa nasugua Unyayo nikitafuta ajira kwa njia ya mtandao au hata ana kwa ana. Nimekua mhanga wa ajira mpaka nimekata tamaa.
Kutokana na Mimi kuzaliwa kijijini Muda Wangu mwingi wa ziada nimekuwa nikijikita zaidi kuchunguza Mazao ya Kilimo yenye Tija katika Taifa kiujumla.
Kilimo Cha Mazao ya Biashara kama Kahawa, Korosho, Mkonge, Parachichi n.k ni kilimo kizuri ila kinahitaji Sana vitendea Kazi, zaidi Mtaji. Changamoto ya Mtaji ni kama Ukoma kwa nchi yetu kwani vijana Wengi Wana Ideas za Biashara ila wanakutana na changamoto ya Ukosefu wa Mtaji. Nimewaza kwa upana nikakuta tunaweza kufanya Biashara ya Kilimo Cha mbogamboga na matunda kwa Mtaji mdogo na kijana mtanzania msomi ukapata fedha za kuweza kuendesha maisha.
Mfano:- Unaweza kukodi Shamba kama hekari moja ukasia mbegu na kupanda matunda kama Tikiti au Tango, Biashara ya Kilimo inahitaji Subra na kujitoa kukubali kuteseka kwa hali na Mali. zao Hili ni zao la muda mfupi Siku 75-90. Unaweza kuwekeza kwa kiasi Cha shilingi laki Tano Hadi Milioni moja na kama utakuwa umefuatilia vizuri taratibu za kilimo unaweza kupata Mazao mengi na kukupa faida kubwa Sana.
Unaweza kulima Kilimo Cha kutegemea Mvua au Kilimo Cha Umwagiliaji. Kilimo Cha Umwagiliaji ni kizuri na kinamatokeo makubwa ila kinahitaji Mtaji mkubwa kwani Kuna vifaa vya kununua kwa ajili ya Umwagiliaji.
Kilimo Cha Mvua ni Kilimo rahisi ila si Uhakika kwani kinategemea Mvua hivyo endapo Mvua utachelewa kunyesha/kupungua ni dhahiri kwamba mimea itadhoofu au kukauka na kukata makisio.
Kwanini nimeileta Hoja hii kwako? Nimezunguka Sana nikakuta idadi kubwa Sana ya Wasomi mtaani wakipiga soga, kusoma magazeti vijiweni na kucheza Draft Pamoja na Puli table, Kisha Jioni wanarudi kwa wazazi wao kula na kulala. Nafsi yangu huumia Sana lakini nashindwa chakufanya kuokoa vijana wenzangu kwenye hili wimbi la ukosefu wa Ajira.
Tufanyeje basi ili tuweze kuepuka tatizo hili la Ukosefu wa Ajira?
1. Sera ya Elimu itazamwe Upya na Masomo ya Science ya Kilimo yapewe kipaumbele kwanzia Elimu ya msingi Hadi Sekondari.
2. Vijana wapewe Mitaji/Ruzuku ili waweze kujikita zaidi na Shughuli za Kilimo.
3. Mabenki yatoe mikopo ya riba nafuu hususani kwa wakulima ili wakulima waweze kuwekeza kwenye kilimo. Hii itapunguza ukali wa ukata wa Ajira.
4. Mazao ya Biashara kama Kahawa, Korosho, Mkonge, Parachichi yahimizwe kulimwa Kila mkoa kadri inavyowezekana na Maafisa Kilimo yapewe Vitendea Kazi vya kutosha.
5. Viwanda vya kubangua Kahawa/ Korosho au Mkonge vijengwe Kila mkoa unaolima Zao husika.
Hata hivyo kuzaliwa Maskini sio vibaya Ila kufa Maskini ni kosa kubwa.
Andiko hili ni mawazo yangu ya awali tuu, Karibu Ndugu yangu pale penye kuongezea tutayajenga sote. Nipo tayari kupokea mapendekezo yenu.
Nakuomba usisahau kulipigia kura andiko hili. Ahsante.

Upvote
8