Sayansi ya zamani ya kutibu vidonda yafufuliwa na kuhamasishwa

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,265
Kidonda kwenye mwili wa binadamu huchukua muda mrefu kupona kwa sababu hakuna kitu cha kuondoa nyama iliyooza kwenye kidonda hicho. Kwa kawaida daktari wa kidonda husafisha/hukwangua kidonda hicho kwa kutumia chombo maalumu (scalpel).Kufanya hivyo husababisha kidonda kukauka na kupona haraka.

Lakini hapo zamani kabla ya ugunduzi wa matumizi ya scalpel, vidonda viliachwa hivyohivyo.Hata hivyo, ilibainika kwamba vidonda vilivyoachwa hivyohivyo na kuzengewa na nzi wengi,vilionesha dalili za kupona haraka.Sababu ilikuwa nini?

Wauguzi wadadisi waligundua kwamba funza(maggots) wa nzi walisaidia kusafisha kidonda kwa kula uchafu wote wa nyama zilizoozea kwenye kidonda. Na wauguzi hawa waligunduakitu cha zaidi: Kwamba funza wazuri wa kuponesha kidonda ni wale wanaozalishwa na aina ya nzi aitwaye 'green bottle' -yule nzi mkubwa wa kijani anayependa kuishi chooni.

Baada ya ugunduzi huu hospitali nyingi zilijitahidi kutumia njia hii ya matibabu ya vidonda kwa kuanzisha maabara za kukuzia nzi wakubwa wa kijani na kutumia funza wanaozalishwa kama dawa. Amerika, kupitia shirika lake la FDA ilihalalisha matumizi ya funza kwa matibabu mwaka 2004.

Nchini Kenya, hospitali zimeanza majaribio ya tiba hii. SOMA

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…