Sayansi za mchongo

onea 22

Member
Joined
Jul 31, 2020
Posts
34
Reaction score
20
ilikuwa tarehe 25 july 2020 baada ya kuamka asubuhi kwa ajili ya kwenda kwenye mizunguuko yangu ya kila siku nakutana na baridi kali sana. Miaka mingi kidogo wakati nakua kipindi cha baridi kilikuwa ni mwezi wa sita, sasa hii baridi ya mwezi wa saba kwenda wa nane veepe?

Utagundua kitu sawa na hicho pia ukiangalia mvua za masika, mara nyingi zilikuwa nyingi mwezi wa april, lakini kwa miaka ya karibuni mwezi May mvua zinapiga vizuri tuu. Katika kujiuliza kwa nini mambo yanakuwa hivyo? Hizi ni baadhi ya nadhaharia nilizojaribu kuja nazo kuelezea haya mabadiliko.

I)kupungua/ kuongezeka kwa mwendokasi wa dunia kulizunguuka jua
tunafahamu kwamba majira ya mwaka yanatokana na mzunguko wa dunia kulizunguuka jua. Kama mwendokasi wa dunia umeongezeka, maana yake ni kwamba vipindi vya majira ya mwaka vingekuwa vinawahi kabla ya muda wake wa kawaida. Kwa mfano msimu wa baridi tungekuwa tunauona mwezi wa tano.

Lakini kitu hiki ni vigumu kutokea kwani kunahitajika chanzo cha kuiongezea dunia mwendokasi na hakionekani kwa kweli. Pia kutokana na kesi tuliyonayo kwa sasa ya majira kusogea mbele kidogo ya muda wa kawaida inathibitisha kwamba dunia haijaongeza mwendokasi.

Kwa upande mwingine kama mwendokasi wa dunia kulizunguuka jua ungepungua basi maana yake majira ya mwaka yangekuwa yanasogea mbele kutoka kwenye yale ya kawaida kama tunavyoona sasa. Nadharia hii pia ina uwezekano mkubwa wa kuwa kweli kwa sababu kuna sababu nyingi za kusababisha mwendokasi wa dunia kupungua kwa kiasi kidogo kidogo.

II)kuongezeka kwa mzingo wa obiti ya dunia kulizunguka jua

Hapa pia kama mzingo wa obiti ya dunia utaongezeka maana yake ni kwamba dunia itatumia muda mwingi zaidi kulizunguuka jua na kupelekea kubadilika kwa majira ya mwaka kutoka tulivyozoea hapo nyuma.

Kwa kumalizia kama nadharia nilizozitaja hapo juu ni sahihi basi kuna mambo mengi duniani yanakwenda ndivyo sivyo. Kwa mfano swala la mwaka mpya kama ni kweli mwendokasi wa dunia umeongezeka au mzingo wa obiti ya dunia umeongezeka basi yawezekana siku za dunia kulizunguuka jua zikawa ni zaidi ya siku 366 za awali.

Kwa mabadiliko ya majira ya mwaka kwa mwezi mmoja yawezekana kwa sasa tukawa tunakamilisha mwaka kwa siku 367 au zaidi. Kama tukichukulia kwamba siku moja inapungua kila mwaka kwa miaka 30 majira yanaweza kuhama kwa mwezi mzima.

BY SIOGOPI
 
Kuna mambo memgi yanachangia, uharibifu wa mazingira ukiwa sababu moja wapo.
 
Kwa mantiki yako hiyo ya kupungua kwa kasi ya dunia kulizunguka jua na kuongezeka kwa mzingo wa orbit basi kusingeathiri tu majira ya mwaka bali hata vitu kama urefu wa siku, saa n.k

Je upande huo umejaribu kufanya observation uone kama kuna mabadiliko pia?
 
hapana ndugu, urefu wa siku unatokana na spidi ya dunia kujizungusha kwenye muhimili wake yenyewe,co kama rotation ikibaki kuwa ile ile basi urefu wa siku hauwezi kuathiriwa..,the same applied to masaa.
 
hapana ndugu, urefu wa siku unatokana na spidi ya dunia kujizungusha kwenye muhimili wake yenyewe,co kama rotation ikibaki kuwa ile ile basi urefu wa siku hauwezi kuathiriwa..,the same applied to masaa.
Vipi kuhusu mwaka? Maana yake dunia itachukua muda mrefu zaidi kukamilisha mzunguko mmoja kulizunguka jua. Maana yake siku za mwaka zitaongezeka.
 
Vipi kuhusu mwaka? Maana yake dunia itachukua muda mrefu zaidi kukamilisha mzunguko mmoja kulizunguka jua. Maana yake siku za mwaka zitaongezeka.
ndio maana nimeandika huu uzi, inawezekana sisi tunasema kuwa mwaka umeisha kumbe bado au tayari ulishapita sisi ndio tunasherehekea mwaka mpya..

Nilichotaka tuangalie zaidi ni kuwa huenda tumepoteza hesabu ya muda. Maana kwa kifupi mwaka mmoja ni muda tunaoutumia kulizunguka jua. Tukikamilisha mzunguko mmoja huo ni mwaka kwa mfano ukiwa kwenye sayari ya mercury, unaweza kutimiza mwaka ndani ya siku 88, ambazo hapa kwetu ni miezi mitatu tu, dunia yenyewe inatumia siku 365 (tunaambiwa). Lakini je, spidi yetu iko vile vile haibadilikiii hata kidogoo? Na njia tunayopita kuzunguka jua ni kweli hatuyumbi hata kidogo. Mabadiliko kidogo tu ya hivi vitu yanaweza kuleta mabadiliko makubwa ndani ya miaka lets say 1000.
 
Vipi kuhusu mwaka? Maana yake dunia itachukua muda mrefu zaidi kukamilisha mzunguko mmoja kulizunguka jua. Maana yake siku za mwaka zitaongezeka.
Unahakikishaje kuwa dunia imekamilisha mzunguko au unafata tarehe zilizowekwa?
 
Lakin kuna wananzengo wanasema binadamu ana athari ndogo mno kuweza kuathiri mabadiliko ya hali ya hewa na muda duniani.kwamba ishu za global warming pia ni event/situation ambazo ni well planned na wenye dunia yao.kwamba kuna mvua za kutengeneza,matetemeko nk
NB: nahisi ni nje ya mada
 
Watu wanaojua maswala ya nyota na mambo ya anga kwa ujumla, wanaweza kutufafanulia zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…