Unatafita ubishani tu! Unajua speed inasomwa kwenye nini? Pikipiki ukiiangalia imeandikwa speed meter inaenda hadi 120 unadhani hiyo 120 ni sawa na ya gari? Ukikaa kwenye gari iwe speed 120 ule upepo mwenye pikipiki angeweza kuhimili? Usidanganywe na maandishi wewe!! Speed inasomwa kwenye mzunguko wa gearbox so gari kubwa na ndogo hazifanani hilo tambua.. Nimeshaongozana sana na gari ndogo kwenye 50kph wakinifata mimi wanapigwa tochi na mimi nikifata 50 yao kwangu nakuwa 40kph au 44kph.. Ule mzunguko wa gearbox na tairi zikiwa kubwa itafanya mzunguko mmoja wa gari kubwa uwe tofauti na wa gari ndogo coz gearbox yake ndogo hadi tairi mzunguko ni mdogo, so tairi za scania ikienda mara 2 wewe itakubidi izunguke mara 3 ndo tutakuwa sawa maana yake kwenye kipimo cha speed utakuwa juu kuliko mimi mwenye gari kubwa... Ufahamu kuwa mimi nikiwa speed 110 ili unipite utatakiwa uwe zaidi ya 140 na gari yako
Si kwamba ninakukosoa.....ila naomba urudi kisoma tena kitu kinaitwa gear ratio....
Waliotengeneza magari makubwa na madogo walitumia physics na hisabati za hali ya juu...
Hapa kinachotokea ni nini...
Kwa mfano Scania ikiwa 50kph na Passo ikiwa 50kph, haya magari mawili hayataachana kwa kwa mendo. tofauti itakuwa kwenye mzunguko wa gear box na matairi..
Ni dhahiri kuwa gear box ya gari kubwa itakuwa na mzunguko medogo kwa sababu ina matairi makubwa na gear box ya gari ndogo itakuwa na mzunguko mkubwa ili kufanya katairi kadogo kazunguke sana ili ku... maintain speed iliyopo..
Kwa hiyo, kwa mfano tairi la gari kubwa likizunguka mizunguko 2 ili kupata speed 50, tairi la gari mdogo linaweza kuzunguka mizunguko 3....
Hapa ni swala la namna gear zilivyotengenezwa...
Kwa hiyo si kweli kama watu wanavyopotoshana vijiweni kuwa basi likiwa mf 100kph, passo iwe 120kph eti ndiyo ziwe sambamba,......ni upotoshaji..
Gari kubwa na ndogo yote yataenda sawa kama yapo speed 100 tofauti itakuwa kwenye idadi ya mizunguko ya tairi na gear ratio...
Kuna mambo machache yanayoweza kuathiri speed halisi ya gari na ndiyo maana kwenye tochi wameweka balansi ya zile points 5.....yaani ukiwa speed 50.5 kurudi chini huandikiwi faidi....
Kwa mfano gari ndogo kama ilitoka na tairi size 175/70 r15, ukaja ukabadilisha ukaweka 195/70 r14....hapa utapata badiliko la speed bila wewe kujua....ndani kwenye dash utaona mshale unasoma 50 lakini actual speed kwa nje ukipihwa tochi inaweza kuwa 50.2 mpka 50.3 hivi....kwa ninj..? kwa sababu umebadilisha ukubwa wa tairi uliopimwa kulingana na gear ratios za gari husika na kuweka tairi kubwa........
Nawasilisha.