Kuna kozi za MD zinatolewa Tanzania kwa udhamini wa bodi ya mikopo (HESLB). Hivyo wala usiwe na presha, presha iwe kwake kufaulu sana ili apate admission. Vyuo vizuri kwa sasa ni Muhimbili (competition kubwa kupata), zikifuatiwa na KCMC na Bugando. Ukiwa na sifa na ukapata nafasi huko utapata ushamini wa bure toka bodi ya mikopo.
Kuna scholarships za kusomea degree hizo hizo nchini China, Urusi, Uturuki na Algeria. Sijui kama Misri na Cuba kama wanatoa. Ulizia Wizarani kwa Kawambwa na balozi za nchi tajwa.
Ukiacha Misri, ni bora mdogo wako asome hapa hapa Tanzania, kwani ukipelekwa katika hizo nchi tajwa utasajiliwa kwenye vyuo vidogo na mara nyingi graduate huwa hayuko vizuri kitaaluma.
BTW: Huyo dogo anataka kusoma Medicine au wewe ndio wataka asomee Medicine? Vichwa vingi sana vipo kusoma PCM na PCB, galafu vinafikiria engineering tu na Medicine. Wenzenu mnaowaona mazezeta sasa bdio wanakuja kuwatengenezea policies na hata pia kuwapangia mishahara. Ukisoma na kufaulu vizuri PCB na PCM si lazima usome Medicine au Engineering. Kuna course nyingine nzuri kama Bcom, Bpharm, Economics n.k.