Masalu Jacob
JF-Expert Member
- Jul 26, 2017
- 1,013
- 1,183
Tanzania ! Tanzania !
Habari za muda huu wananchi wenzangu vipenzi vya Taifa letu Tanzania !
Naomba kutoa wazo na mchango wangu kwa Wizara ya Elimu Tanzania. Ikiwapendeza tunaomba huduma ya Usafiri kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari za Serikali nchi nzima haijarishi Jiografia ya eneo. Watoto wanateseka sana na usafiri hasa kutoka maeneo wanakoishi mpaka shule wanakosomea.
1. Kila Kata pawe na Basi 4 za kutoa huduma za Usafiri kwa Wanafunzi wa Shule za Serikali pekee. Idadi inaweza kuongezeka kutokana na wingi wa wanafunzi husika.
a) Wananchi tutachanga Elfu 7,500/= kwa mwezi kwa kila mtoto kwenda - rudi.
b) Gharama za Huduma za Magari ni Serikali mtakomaa wenyewe
c) Dereva na Konda watakuwa waajiriwa wa Halmashauri husika kwa ajira mkataba au kudumu mtachagua wenyewe kutokana na mapato ya Halmashauri.
2. Kwenye hayo Mabasi Walimu wasipande kabisa hata raia yoyote haijalishi hadhi yake. Huu ni usafiri wa watoto wa Shule tu. Hata wanafunzi wa wa Shule Binafsi wasiruhusiwe kupanda abadani.
3. Namna ya upatikanaji wake wa hayo Mabasi mtatujulisha ila tusichangishwe hata kidogo maana hayo ni sehemu ya majukumu yetu kuleta ustawi kwa jamii na maendeleo.
Karibu.