Wabongo kwenye topics muhimu kama hizi huwapati, ungeweka Jerry Muro au Kova au Kikwete au ufisadi kwenye kichwa aaaah, wangejazana hapa kama nzi kwenye soko la samaki.
Ahsante sana, natumai tutapata dawa au chanjo katika miaka michache ijayo.
Dawa ikipatikana usipapatike mara moja kujiachia. Kwanza haitatatolewa bure mpaka watengenezaji watakapokuwa wame-recover investment yao. Kwa hiyo kwa sisi nchi masikini itatuchukua miaka mitano mpaka kumi toka kugunduliwa kuweza kuzinnunua kwa bei tunayoweza kumudu. Dawa za kupoza tunazotumia huku sasa hivi huko kwao wameishaziacha kwa sababu ziko mpya bora zaidi. Lakini kwetu hazijafika.Pamoja na jitihada zote hizo swali ninalojiuliza itakuwaje siku hiyo wakitangaza kuwa dawa ya HIV/AIDS imepatikana? Sipati picha...hebu niwazueni wana JF...
Pamoja na jitihada zote hizo swali ninalojiuliza itakuwaje siku hiyo wakitangaza kuwa dawa ya HIV/AIDS imepatikana? Sipati picha...hebu niwazueni wana JF...