Scooter za kichina kama TVS Jupiter, changamoto zake nini?

EHK

Member
Joined
May 19, 2011
Posts
74
Reaction score
96
Habari,

Naulizia kwa mwenye uzoefu wa hizi scooter za Kichina, TVS Jupiter (sina uhakika kama kuna models, brand nyngne) ambazo kwa mwonekano ni kama Honda Click ama Yahama. Changamoto yake hasa ni nini na durability yake ipoje, nipo interested kutafuta moja kwaajili ya town trips za kila siku.

Honda Click nadhani ni nzuri zaidi ila bei yake ipo juu kidogo ambapo siwezi kuafford kwa sasa.

Nimeattach picha kwa mwenye kujua hasa zinafananaje.

Natanguliza shukrani.

 
Iko hivi...
Honda Click:
!: Nyingi ni used kwa hiyo zinakuwa na changamoto, mpya zina bei ya IST
2: Service yake ni gharama, Engine oil (14,000), Gearbox oil(9,000), Air cleaner(15,000), coolant 10k +, ikitoa moshi tu..baba uza
3: Haihitaji rough road
Kiufupi, service yake na spare zake ni bei sana.
Haojue /Sanya /Loncin /King lion n.k 110
1: Hizi ni mpya kabisa
2: Service yake bei chini, na kama wewe sio gegedu, itakuchukua 5 yrs kubadili spare
3: zinapeta hata rough road
4: Spare zinaingiliana na bei ipo chini sana

NB: Kama uchumi wako ni tia maji tia maji...chukua hizo za kichina zinauzwa around 2.5m (Haojue na Loncin naona zinapeta sana)
 
Nimejaribu kupitia google nimeiona tvs Jupiter, ila haijafana na Click.
Tvs iliyofanana na click inaitwa TVS Ntorq.
Tvs pikipiki zao ni nzuri na wanajitahidi kutengeneza model zinazofanana na brand kubwa kama Honda, Yamaha n.k
Tvs wanazo pikipiki mpaka zenye CC 800, ila tatizo hizi pikipiki zao kwa bongo ni vigumu sana kuzikuta madukani nyingi zilizopo ni haya mabodaboda.
Hii chini ni Tvs Jupiter
 
Tvs wanayo mapikipiki makubwa yanaitwa Apache.
Ukiachana na brand za Japan na Europe TVS wanajitahidi sana kutengeneza models nzuri, ila kwa bongo sijui kwa nini hawazileti.
 
Shukran, maelezo yameshiba kabisa.
 
Yes hyo picha ni kati ya model zao, ila zipo zinazofanana na Click pia
 
Kuna jamaa anapitaga nayo mtaani kama hii inapendeza sana ina rangi ya brown bado mpya kabisa
 
Hivi vidude vina uhusiano gani na jamaa wa kipemba mbona wanavipenda sana???
 
Hivi vidude vina uhusiano gani na jamaa wa kipemba mbona wanavipenda sana???
Vya wapemba ni honda click au honda Vario.
Wapemba/Wazanzibari wana historia ya muda mrefu na scooter, kuanzia zile mimba za mbuzi za kuendea marikiti mpaka haya matoleo ya siku hizi.
Kikubwa hizi scooter zinatumika kwa safari fupifupi za hapahapa mjini, ulaji wake wa mafuta ni mdogo, ni imara sana ingawa spear zake kidogo ni ghali, kikubwa zaidi hizi pikipiki ni za automatic hivyo hazina usumbufu wa kuhangaika na clutch na kuchange gear.
 
Samahan wadau, vipi changamoto ya hizi pikipiki ndogo maarufu kama 110 ,, kwa upande wa spea na ubora wa chombo chenyewe

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…