Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Hii achatuseme kwamba kazini kwa Diddy kuna kazi. Kesi zinazidi kumiminika zinazomuhusu yeye hadi sasa ni maumivu kwake na je atazishinda zote kesi hizi?
==================
Mkali wa Hip-Hop wa Marekani, Sean “Diddy” Combs anatuhumiwa kuhusishwa katika kesi mpya 120 za unyanyasaji wa kingono zinazotarajiwa kuwasilishwa mahakamani siku 30 zijazo kabla ya kesi zake za awali kuanza kusikilizwa.
Akiongea na waandishi wa habari jana Oktoba Mosi, wakili Tony Buzbee kutoka Texas ameweka wazi kuwa watu 120 wamewasilisha madai ya unyanyasaji wa kingono unaodaiwa kufanyika miaka 20 (miongo miwili) iliyopita huku akisema kuwa ana ushahidi wa picha na video.
Aidha wakili huyo alimtaja mhusika mmoja kuwa ni mtoto mwenye umri wa miaka tisa ambapo Diddy na wengine wanatuhumiwa kumnyanyasa kingono katika studio za Bad Boy Records huko New York.
Soma Pia:
Hata hivyo Diddy anapambana kujinasua kutoka kwenye mikono ya sheria baada ya kukusanya wanasheria mashuhuri kuhakikisha wanamtetea na kupata dhamana ya kutoka mahabusu zikiwa zimepita wiki mbili tangu alipotiwa nguvuni.