Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Sean "Diddy" Combs ameripotiwa kuondolewa kwenye uangalizi wa kujitoa uhai huku akiendelea na maandalizi ya kesi yake ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya biashara ya ngono. Kwa mujibu wa wakili wake, Diddy yuko "imara na amewekeza muda mwingi kwenye utetezi wake."
Diddy, ambaye yupo kwenye jela ya Metropolitan huko Brooklyn, New York, alikamatwa Septemba 16 na kushtakiwa kwa makosa ya kusafirisha binadamu Kwa ajili ya biashara ya ngono, kuwatumikisha kwa nguvu, utekaji nyara, na ulaghai.
Hapo mwanzo, Diddy aliwekwa kwenye uangalizi wa kujitoa uhai kama hatua ya tahadhari, lakini sasa amejitayarisha kukabiliana na kesi hiyo huku akiendelea kusisitiza kuwa hana hatia.
Diddy pia anakabiliwa na mashtaka ya zamani kutoka kwa aliyekuwa mpenzi wake, Cassie Ventura, aliyemshtaki kwa unyanyasaji wa kijinsia, ingawa walifikia makubaliano ya usuluhishi siku moja baada ya kufungua kesi hiyo.