Secondary infertility [ ugumba baada ya kushika mimba ]

Secondary infertility [ ugumba baada ya kushika mimba ]

Trayvess Daniel

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
651
Reaction score
1,244
SECONDARY INFERTILITY:

hii ni aina ya ugumba ambao hutokea baada ya mtu kushika mimba moja au zaidi. Imekuwa maarufu kuliko ugumba wa kushindwa kushika mimba kabisa. Huu unasababishwa na mambo mbalimbali mengi yao yakichangiwa na maisha ya kila siku. Hii huchangia utokaji mimba wa mara kwa mara.

KWA WANAWAKE:
Hali hii hutokea kipindi ambacho yai limeshindwa kufikia eneo la urutubishwaji, yai likishindwa kujishikiza kwenye ukuta wa mimba, ovari zikiwa na shida ya utoaji mayai na sababu nyingine kadhaa

VISABABISHI:
Nitataja visababishi vichache vinavyogusa watu wengi. Ulaji mbaya, uzito kuzidi au kupungua, hormonal imbalance, uvimbe au nyama zinazoota kwenye kizazi, uvutaji sigara, dawa za mionzi, cancer ya kizazi, unywaji pombe kupitiliza, umri, kisukari na magonjwa ya zinaa na sababu nyingine nyingi.

KWA WANAUME:
Hii mara nyingi hutokana na matatizo upande wa mbegu za kiume au mbegu kushindwa kusafiri kutoka zinakotunzwa mpaka kutolewa [blockage]

VISABABISHI:
mengi ni kama ya upande wa kike ukiongeza erectile dysfunction na baadhi ya njia za uzazi wa mpango kama vile vasectomy.
Mwenye maswali aulize na mwenye uelewa zaidi kuhusu topic husika atujuze zaidi.

TAKE HOME: Tupende kuishi maisha ambayo ni rafiki kwa afya.. ulaji mzuri, mazoezi, unywaji pombe kiwango kinachoshauriwa n.k
Kwa wenye hili tatizo wawaone wataalamu na mwliopona tatizo hili watuabie walipona vipi.
 
hili ni tatizo kubwa sana kwenye jamii yetu........
 
hili ni tatizo kubwa katika jamii yetu na ni chanzo cha ndoa nyingi kuvunjika
 
Back
Top Bottom