Seedless Orange haina uhusiano na GMO, ni historia inakataa kabisa

Seedless Orange haina uhusiano na GMO, ni historia inakataa kabisa

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Watanzani wengi kwanza tukubali hatuna elimu ya GMO zaidi ya story za vijiwe vya kahawa na Tangawizi huko ndio tunalishana matango poli, Pia kwa uelewa wetu mfinyu tunazania GMO ni mazao yasio kuwa na mbegu, hizi ni akili za kijinga sana.

SEEDLESS ORANGES

Seedless Oranges ambayo ni navel orange ni matokeo ya mutation katika shamba moja la Wareno katika sehemi inaitwa Bahia huko Brazili, hii tunazungumzia karine ya 19 huko miaka ya 1810.Hii mutation ilisababisha mti huo kutoa machungwa ambayo ni seedless, na baada ya hapo ndio wakaanza kufanyia budding huo mti na kuotesha zaidi na zaidi na kusambaza.

GMO techinolojia yake.

Herbert Boyer na Stanley Cohen ndio watu wa kwanza kufanya mageuzi ya vina saba kwenye kiumbe hai mwaka 1973, hio miaka tiyali Seedless oranges ziko sokoni.

Kuna baadhi ya maeneo hata hapa Tanzania hasa kwenye mission walipo kaa wazungu miaka ya kitambo kulikuwa na machungwa seedless. Binafisi nimeyala kwenye mission fulani miaka ya 1988 huko.

Na kwenye mimea GMO imeanza juzi juzi kati hapa.

Pia jua kwamba GMO sio kwa kila mimea, wale jamaa wanafanya biashara na hawazalishi GMO kwenye mazao ya muda mrefu, GMO biashara yao kubwa ni kuuza mbegu na ndio maana utaona mazao wanayo dili nayo ni yale ya kila msimu unaenda kununua mbegu. GMO sio wehu wazalishe mbegu za mimea inakaa miaka 30 sasa watafaidika vipi?

Mwisho kabisa.
Si kwamba kila kitu kisicho kuwa na mbegu sasa ndio GMO yenyewe, na chenye mbegu sasa ndio OG,historia ya seedless grapes ni ya miaka ya 1600 huko ukanda wa Medtreranian.Kwenye record za GMO bado hawajaweza zalisha machungwa na sio machungwa tu na mimea mingine. Hadi sasa kwenye matunda ni Apple, kuna Papai na tikitiki maji kama sijakosea.

Screenshot_20250216_211148_com.android.chrome.jpg


Hio hapo ni Papai ya GMO huko Hawaii Marekani, sasa kibongobongo na story za vijiweni hio ni OG make tunajua GMO ni kitu ksiimcho kuwa na mbegu,
 
Je GMO inamadhara yyte kwa mlaji mana Kuna jamaa huko TikTok kanitisha Ile mbaya anasema tikiti za skuiz ni hatari kwa afya ya uzazi hasa kwa mwanaume.
 
Back
Top Bottom