Sehemu kadhaa za kuwa makini nazo hususani kipindi cha mlipuko wa magonjwa

Sehemu kadhaa za kuwa makini nazo hususani kipindi cha mlipuko wa magonjwa

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Wakati tukiendelea kujikinga na maambukizi ya virusi vya #Corona tumekuwa tukielezwa umuhimu wa kuosha mikono kwa maji tiririka na Sabuni au kwa kutumia vitakasa mikono “sanitizer”.

Mbali na kusafisha mikono yetu, kuna vitu ambavyo ni muhimu pia kuvisafisha kwa dawa maalum “disinfectant” ili kuua vijidudu kwani ni vitu ambavyo tunavishika kila mara na ni rahisi kuhamisha vijidudu kwenda kwenye mikono yetu hata kama tumeiosha.

1. Simu
Ni wazi kuwa Wengi wetu tunashika simu zetu kila dakika. Simu huweza kukaa na vijidudu kwa muda mrefu sana hivyo ni muhimu kuzifuta kwa dawa au tishu zenye dawa kila tuwezapo.

2. Kompyuta na vifaa viambatanavyo
Hii ni kwa wanaofanya kazi nyumbani na hata maofisini. Inawezekana ukashika sehemu yenye maambukizi na kisha kushika kompyuta yako, kipanya au 'keyboard' hivyo jitahidi kuvifuta ili kuua vijidudu.

3. Rimoti
Rimoti za televisheni, AC, feni, vifaa vya kuchezea games ni sehemu ambazo vijidudu vinaweza kujificha kutokana na kushikwa kila mara na watu mbalimbali.

4. Vitasa, Mabomba, Swichi za taa, sehemu ya kuflashi choo
Sehemu hizi huguswa na watu wengi hususani sehemu za jumuiya kama ofisi, hospitali na Nyumba za familia kubwa. Inashauriwa kuwa na ratiba ya Kuvifuta ili kuzuia kusambaa kwa vijidudu.

5. Meza
Iwe ya kulia chakula au ya kuwekea vitu au ya jikoni, meza ni sehemu itumikayo sana, ni sehemu ambapo wengi huweka mikono. Safisha meza mara kwa mara kwa dawa maalum hususani kama una watoto eneo husika

6. Vifungashio vya vyakula
Katika mlipuko wa magonjwa ni kawaida kuagiza vyakula mtandaoni ili kuepusha kutoka nje. Wakati hii ni njia salama lakini huweza kuwa njia ya vijidudu kuingia nyumbani kwako. Safisha kifungashio kulingana na aina yake au hamisha chakula kwenda chombo kingine na utupe kifungashio kisha kunawa mikono yako.

7. Mikoba
Kwa wanaotoka sehemu moja hadi nyingine, mkoba huweza kubeba vijidudu kutokana na unapouweka. Kwa kipindi cha magonjwa ya mlipuko ni vyema kuwa makini na mikoba na waleti na kuzifuta ili kuua vijidudu.

8. Usukani na mlango wa gari
Kwa wenye magari hizi ni sehemu ambazo utazishika mara nyingi sana kwa siku. Unapotoka sehemu kadhaa na kushika vitasa, sehemu utakazoshika za kwanza ni hizo. Pia kwa usafiri wa umma kama 'uber' ni muhimu dereva kusafisha kifungulia mlango nje na ndani kila baada ya mteja kushuka.
 
Upvote 2
kwani hivyo virusi vina uwezo wa kua hai kwa muda gani ????
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom