SoC03 Sehemu tajiri kuliko zote ulimwenguni, taifa tajiri la Tanzania 2050

SoC03 Sehemu tajiri kuliko zote ulimwenguni, taifa tajiri la Tanzania 2050

Stories of Change - 2023 Competition

Mzee wa Kosmos

New Member
Joined
May 30, 2023
Posts
3
Reaction score
2
UTANGULIZI
Miaka 7 iliyopita niliamua kufanya uchunguzi na tafiti mbalimbali kwa nini mataifa mengi sana ya afrika ni masikini pamoja na taifa letu la Tanzania. Katika uchunguzi na tafiti zangu niliamua kusoma historia ya ulimwengu wa kale,nikasoma na ulimwengu wetu wa sasa na nikasoma ulimwengu unaokuja,pia nikasoma nini kinatofautisha taifa moja na taifa lingine. Kabla sijaja na maoni au mapendekezo nini kifanyike hili tuweze kutatua matatizo na changamoto zilizomo afrika na taifa letu ni muhimu tujue nini maana ya taifa,pia tujue maana ya neno nchi,pia tujue sehemu tajiri kuliko zote ni nini ?

NINI MAANA YA TAIFA
Taifa ni jumla ya mifumo yote inayoongoza,inayoendesha,inayotawala,inayoshawishi,inayoathiri maisha ya watu na vitu vyote vilivyomo kwenye nchi.Kila taifa hapa duniani linaongozwa,linatawaliwa na kuendeshwa na mifumo. Ubora wa taifa inategemeana sana na ubora wa mifumo iliyomo kwenye taifa hilo.Na ubora wa mifumo unategemea sana ubora wa maarifa na ujuzi ndani ya akili za watu wanaoendesga mifumo hiyo.Ukisoma historia na kufanya uchunguzi utakuja kuelewa kuwa mataifa yaliyokuwa na nguvu katika ulimwengu wa kale,ulimwengu wa sasa ni mataifa yote yalio na mifumo imara ya sayansi na teknolojia,mifumo imara ya kisiasa ,mifumo imara ya elimu na kadharika.Mataifa mengi ya afrika yanashindwa kutimiza malengo zake kwa sababu ya mifumo isiyokuwa imara.Maarifa na ujuzi sahihi ndani ya taifa ndio uimara wake,kwa sababu maarifa au ujuzi ndio unatoa nguvu kwa ajili ya kuendesha mifumo hiyo.

SEHEMU TAJIRI KULIKO ZOTE
Kama tatujua siri hii tunaweza kutatua zaidi ya asilimia 80 ya matatizo kwenye taifa letu la Tanzania ambayo yatatokea baadaye.
Miaka 7 ya utafiti na uchunguzi nimekuja kuelewa kuwa sehemu tajiri kuliko zote duniani ni kwenye akili ya mtu au kwenye nafsi au moyo wa mtu,kwenye akili au moyo wa mtu ndio sehemu ambayo vitu vyote vilivyokuwepo huko nyuma vilitokea uko,vitu vyote vilivyopo sasa vimetoka uko na vitu vyote ambavyo vitakuja kuwepo baadaye vitatokea huko,Maarifa yote ,ujuzi wote ,ufahamu wote,mawazo yote ,maono yote yanayoongoza ,yanayotawala na yanayoendesha maisha ya watu na vitu vyote vilivyomo kwenye nchi yametoka ndani ya akili au moyo wa mtu.Kwenye moyo au akili ndiko sehemu ambayo Imani ya mtu,matarajio ya mtu ,mapenzi ya mtu ,matakwa ya mtu,falsafa ya maisha ya mtu,shauku ya mtu,motisha ya mtu,maono ya mtu,ndoto za mtu,chemichemi za uzima za mtu,malengo ya mtu,kipaji cha mtu ,makusudi ya mtu ukaa uko.Ndani ya akili au moyo wa mtu ndiko mifumo yote inayoendesha serIkali utokea huko.Vitu vyote vimetengeneza,vimeundwa na kuumbwa kupitia akili au moyo wa mtu.Kutokana na sifa ya akili au moyo wa mtu kutoa vitu vyote tunavyoviona na dhamani zote tunazoziona inafanya moyo au akili ya mtu kuwa sehemu tajiri kuliko zote duniani na ulimwenguni kwote.

MOYO AU AKILI YA MTU NI NINI? NA NINI KINATOA UTAJIRI NDANI YA MOYO AU AKILI YA MTU ?

Wanafalsafa ,wanasayansi na wanasaikologia baada ya kusoma asili ,sifa na tabia za mwanadamu wamekuja kugundua kuwa mwanadamu ni mtawala juu ya mazingira yake na vitu vyote.Mwanadamu anatawala mazingira na vitu vyote vilivyomo kwenye mazingira kwa kupitia maarifa na ujuzi unaotoka ndani ya moyo au akili yake .

Moyo au akili ya mwanadamu ni nini?
Ni kipawa au uwezo uliupo kwenye nafsi ya mtu unaomwezesha mtu kufikiria,kupanga,kuelewa na kujifunza vitu vyote vilivyomo kwenye mazingira na kutatua matatizo au changamoto zote zilizomo kwenye mazingira.Moyo au akili ya mtu hili iweze kufikiria au kuelewa mazingira yake inahitaji maarifa au ujuzi kutoka kwenye mazingira na maarifa haya yanapatikana kwenye mazingira na yanaingia kwenye moyo au akili ya mtu kupia milango ya fahamu (masikio,macho,pua,ulimi na ngozi).Hatima ya taifa lolote inategemea sana na aina gani ya ujuzi au maarifa ambayo yanaingia kwenye akili au moyo ya mtu kupitia milango ya fahamu kwa sababu ndio misingi ya akili au mioyo ya watu kufikiri,kuelewa,kujifunza vitu vyote vilivyomo kwenye mazingira na kutatua matatizo yao yaliyomo kwenye mazingira na kwenye taifa hilo.Mafanikio au kuishindwa kwa taifa hilo inategemea sana aina ya maarifa yanayoingia ndani ya akili au mioyo ya watu.Maarifa sahihi yanafanya akili au mioyo ya watu ifikirie sahihi na akili za watu zikifikiri sahihi basi zitapanga,kuamua na kufanya vitu ambayo ni sahihi na maarifa yasiokuwa sahihi yanapoingia kwenye akili au moyo wa mtu yanafanya asifikiri sahihi,kama ufikiri wa akili za watu usipokuwa sahihi utapelekea watu wapange na kufanya mambo ambayo sio sahihi hivyo kufanya vitu ambavyo sio sahihi

KITU KINACHOTOA UTAJIRI NDANI YA MOYO AU AKILINI
Mtu ni mawazo yake na mawazo ndio msingi wa kufikiri kwake.Mtu awezi kufikiri bila kuwa na mawazo .Hili mtu atende jambo lazima afikirie.Hili mtu atende mambo sahihi lazima afikirie sahihi na hili afikirie sahihi lazima awe na mawazo sahihi.Akili au moyo wa mtu ndio unaotawala mwili kupitia ubongo. Akili au moyo wa mtu unatumia mawazo kuendesha na kutawala mwili wa mtu.Mawazo yaliyo ndani ya akili au moyo wa mtu yanatoka nje kupitia maneno yake na matendo yake.Hivyo maneno na matendo ya mtu ndio yanatengeneza mifumo yake ya maisha yake.Mawazo yanatoka nje ya akili ya mtu kama maarifa na ufahamu,matendo yanatoka nje ya mwili wa mtu kama ujuzi.Ujuzi,maarifa na ufahamu ndio vitu pekee vinavyotoa utajiri ndani ya moyo au akili ya mtu kuja kuwa vitu .Vitu vyote wanadamu walivyotengeneza vilikuwa ndani kama mawazo na vimetoka nje ya akili zao kupitia maarifa ,ujuzi na ufahamu ,mifumo yote inayoendesha na kutawala maisha ya mwanadamu inawezesha na maarifa na ufahamu kutoka ndani ya akili au moyo wa mtu,fikiria mifumo yote ya serikali inaendesha kwa msaada ya maarifa na ujuzi kutoka ndani ya moyo au akili ya mtu.Ufunguo wa kutoa utajiri ndani ya moyo au akili ya mtu ni kuingiza mawazo sahihi na kweli kupitia milango ya ufahamu (masikio,macho,pua,ngozi na ulimi),vitu hivi ndio vinabeba mawazo kutoka kwenye mazingira na kuyaingiza ndani ya akili au moyo wa mtu .

TAIFA YA TANZANIA 2050
Kulingana na sensa ya makazi ya mwaka 2022 tanzania ilikuwa na watu milioni 61,741,120.Mwaka 2044 wanakasema idadi ya Tanzania itakuwa mara mbili,kwa maana hiyo kutakuwa na watu Zaidi ya milioni 123 na mwaka 2050 kutakuwa na watu Zaidi ya milioni 130 .Kwa sasa tunaishi kwenye kipindi cha kidijitali,kulingana na watu wanaotabiri mambo ya baadaye wanasema kipindi hiki kitaenda kuzalisha mifumo mipya ya uchumi na mifumo hiyo itategemea sana uwepo wa maarifa na ujuzi sahihi ndani ya akili au mioyo ya watu

HITIMISHO
Kama mtanzania ninayependa taifa langu ,ufunguo wa tanzania mpya ya baadaye ya miaka 30 ijayo ni watoto wadogo,vijana na mifumo yote inayoingiza mawazo au ujuzi au maarifa ndani ya akili za watoto na vijana(mifumo ya elimu ).Kama tutaingiza mawazo sahihi na kweli ndani ya mioyo au akili za vijana na watoto tunatengeneza misingi imara ya taifa la baadaye na Tanzania itakuwa msaada wa mataifa mengi ya Afrika kama ilivyokuwa kipindi (mambo yalikuwa mengi sana zaidi ya page 20 sema kwa sababu ya ukomo wa maneno taishia hapa).TANZANIA THE NEW SOUL OF AFRICA
 
Upvote 1
Back
Top Bottom