Sehemu wanazopendelea kukaa majini na kuzaliana kwao

Sehemu wanazopendelea kukaa majini na kuzaliana kwao

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
618
Reaction score
1,440
Sehemu wanazopendelea
Kukaa majini.

Ikumbukwe kuwa majini walipopigwa na
kufukuzwa,hawakuzuiwa kuendelea kuishi katika
mgongo wa ardhi,Laa hasha! Bali walitawanywa na
kuzuiwa kuishi katika mkusanyiko, yaani jamii ya
pamoja ( mfano wa binadamu tunavyoishi) ila
waliendelea kuishi katika mgongo wa ardhi,

hivyo
na kufanya maeneo wanayopendelea kukaa
kutofautiana na jamii ya majini. Mfano, mashetani wanapendelea kukaa
chooni,majalalani,njia panda,chini ya miti n.k

Nguvu za majini

Licha ya majini kuaminika kuwa viumbe wenye
nguvu na kuogopeka kwa baadhi ya watu,lakini
ukweli ni kuwa ,hata wao majini wanatofautiana
nguvu ambapo kuna wenye nguvu kubwa na
wajanja(wataalamu) kuliko wengine

Nguvu inaweza kuhusishwa na jamii ya
majini,mfano jamii ya majini wanaoishi angani huwa
na nguvu kubwa kuliko jamii nyingine yoyote ya
majini.

Majini kama subiani,Ruhani,na Ifriti ni majini
wajanja kuliko majini wote,na hawa wote ni
miongoni mwa jamii ya majini wa anga.

Kwa mfano, tunaweza kuona uwezo wao wakati
wa mfalme/Nabii suleimani/solomoni ambapo majini
hawa ndio waliomuahidi mfalme suleimani kuleta kiti
cha enzi cha mfalme Balqis aliyekuwa akitawala na
kuwataka watu wamuabudu.

Vyakula vya majini

Kulingana na maandiko ya vitabu vitakatifu vya
dini,tunaoneshwa kuwa viumbe pekee ambao hawali
ni malaika tu.

Hii inatuthibitiashia kuwa majini si
miongoni mwa viumbe ambao hawali kama
inavyoaminika kwa baadhi ya watu.

Bali majini nao
wanakula ,vyakula vyao hutofautiana kama ilivyo
kwa binadamu.

Utofauti huo unasababishwa na
makabila yao,matabaka,maeneo wanayoishi,sifa
zao

Mfano ,majini wenye sifa nzuri(yaani maruhani),
hawa hula vyakula vizuri na vya halali kuliwa.

Lakini
majini machafu kama mashetani hawa hula damu
za wanyama ,damu za watu
waliokufa ,mizoga ,vyakula vya majalalani n.k

Mfano ni swala la kawaida kwenda kwa mganga
kisha ukaambiwa ulete mbuzi ,au kiungo cha mtu ili
kitumike kama kafara.

Basi hicho ulichoagizwa ni
chakula cha mashetani wa kijini



NGUVU ZOTE ZA ASILI ASILIMIA 💯 ZIMEMILIKIWA NA MUNGU ..
 
Kuzaliana kwa majini
Kama tulivyoona huko nyuma,majini wanasifa
nyingi zinazoshabihiana na zile za binadamu kama
kuzaliana.

Tunaoneshwa katika maandiko ya kuwa ,lait majini
wangaliweza kuonekana kwa macho ya kawaida na
kuchanganyika na binadamu katika maisha ya
kawaida,basi pasingelikuwa hata na sehemu ya
kukanyaga kutokana na wingi wao.

Hii inamaana kuwa majini wanazaliana na ndio
maana wao pia ni wengi.

Tofautin na
binadamu,majini huweza kuzaliana kwa wingi na
kuishi kwa Zaidi ya hata miaka 1000

Majini wa kike wanauwezo wa kufanya mapenzi
na majini hadi 27 kwa siku moja bila kuchoka huku
majini wa kiume wakiwa na nguvu nyingi Zaidi ya
kufanya mapenzi na majini wa kike wapatao 160
kwa siku.

Majini pia wanaweza kujibadilisha maumbo na
kuweza kuingiliana na binadamu na kuzaa watoto
wenye asili ya kibinadamu na kijini,
Mfano, SHIQQ ni jamii ya majini ambao hupatikana
kwa kuingiliana baina ya jinni na binadamu.

Mara
nyingi majini hawa huwa ni dahaifu ukilinganisha na
majini wenye asili kamili ya kijini.

Sababu za majini kuwaingia
Binadamu.

👺

Zipo sababu nyingi za majini kuwaingia` binadamu,ila sababu hizo zimegawanyika katika
sehemu kubwa tatu;
👺 Ikiwa hawapendi mtu,
Jini linaweza kumuingia binadamu kwa sababu tu
limekuchukia.

Kama tunavyofahamu majini tunaishi

nao katika majumba yetu,na tunakutana nao
sehemu mbalimbali tunazopita.

Hivyo jinni
linapotokea kukuchukia hukuingia ili tu kukutesa
na hiyo ndiyo furaha kwake.

Ikiwa limekupenda,
Kama ulivyo wewe binadamu unapompenda mtu
hutamani kuingia katika maisha yake na kuwa mwili
mmoja ,vivyo hivyo kwa majini humuingia binadamu
ikiwa limetokea kumpenda.

Asilimia kubwa ya watu hasa wanawake
hulalamika kuingiwa na majini hasa majini mahaba
n.k ambamo miongoni mwa sababu za kukumbwa
nao huwa ni hii.

👺 Kulichokoza jinni,
Wakati mwingine binadamu huingiwa na jinni
kutokana na uchokozi wake,hii inaweza kuwa kupita
au kukaa sehemu inayopendwa kukaliwa na majini
mfano, katika miti mikubwa, fukwe za bahari,chooni
n.k
Hivyo unapopita na kukaa au kuleta
uchafuzi/vurugu katika maeneo yao huweza
kukuingia ili kukutesa.

👺 Kutumiwa kichawi

Majini huweza kutumwa kichawi na watu wanaohitaji
kukudhuru au kukuharibia mambo yako.

Kwa nini majini hawaonekani?
Tunaambiwa katika vitabu vitakatifu kuwa ,baada ya
kufariki nabii suleimani majini waliomba wapewe
uwezo wa mambo

makubwa matatu;
Waliomba:
👺 Waishi maisha marefu,
👺 Wawe na uwezo wa kubadilika badilika kuwa
kiumbe watakacho,
👺 Wawe na uwezo wa kutoonekana katika macho
ya binadamu.

Mambo hayo walioomba mwenyezimungu
aliwakubalia na baada ya hapo majini waliweza
kuishi miaka mingi Zaidi ya ile waliojaaliwa hapo
kabla ambapo walipewa umri hadi kufikia miaka
1000.

Lakini si hivyo mwenyezimungu aliwakubalia ombi
lao la pili, na hapo wakawa na uwezo wa
kujibadilisha badilisha viumbe tofauti tofauti
kutokana na asili ya jinni mwenyewe.


Wapo waliopewa uwezo wa kujibadilisha
majoka,paka,mbwa,binadamu n.k ingawa maumbo
hayo huwa ni muda mfupi tu ili kukamilisha kazi zao. Na mwisho kabisa wakapewa uwezo wa
kutoonekana katika macho ya binadamu,ingawa
bado uwezo huo haukuwa kamili kwani watu
waliopewa na kufunuliwa siri na elimu kuhusu
majini waliweza kuwaona hata kama hawakutaka
iwe hivyo. Lakini pia sababu ya msingi ya kutoonekana ni
mwenyezimungu mwenyewe kutaka wasionekane ili
kutowadhuru,kuwaogopesha na kuwadanganya
binadamu na mwisho kuzama katika maasi. Majini wanaweza kuonekana katika macho ya
baadhi ya watu baada ya kujibadilisha kutoka
katika maumbo yao ya asili. Mfano ili jinni
lijidhihirishe kwako litatakiwa kuja mfano wa
nyoka,mbwa,paka n.k maumbo ambayo sio ya asili
yao.
 
TABAKA LA MAJINII HINN.

Hii ni aina ya majini ambao wako karibu sana na
wanaishi karibu na binadamu pamoja na
wanyama ,majini hawa wanapotokea na
kujidhihirisha katika macho ya kawaida hutokea
katika umbo la mbwa. Majini hawa wamegawanyika katika makundi
makubwa matatu ambapo:
Wapo wenye mabawa na wana uwezo wa
kupaa angani.

Wenye kutambaa wakiwa katika maumbo ya
nyoka.

Pamoja na wale wasiotambaa au kuruka.
 
BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE ALITUTAJIA MAADUI.

1. UMASIKINI
2.UJINGA.
3. MARADHI.

Akasema Hawa ni maadui wa kweli kweli katika hili Taifa.

LEO 2024 BAADA YA MIAKA 60 TUMEKUWA NA MAADUI WENGI ZAIDI.

2024 maadui wameongeseka Zaidi kuliko wale watatu wa 1961.

1.Umasikini na ufukara.
2.Ujinga na upumbavu.3.Magonwa na Maradhi
4.Mmomonyoko wa Maadili.
ushoga, usagaji Kamali, sugar mamy, sugar Dady mashangazi
5 AJIRA
5. Rushwa na Upendelo

6. USimba na u yanga.
7. Mitandao ya kijamii Tiktok, x, nk
8. Manabii wa uongo na Mashehe Uchwara.
9. Ajali nyingi mno.
10. Gharama kubwa za maisha, ujenzi holela nk

MAMBO NI MENGI SANA VIJANA WA KITANZANIA WANAWAZA MAMBO YA HOVYO SANA SIMBA NA YANGA ZINATAWALA MIKEKA NK.

OKOENI TAIFA LENU LEO.
MKIFIKA MBINGUNI MTAHOJIWA NA MUNGU MLILIFANYIA NINI TAIFA LENU NIMEMALIZA.
 
Back
Top Bottom