Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Usafi wa nguo hufanyika kila mara na hii inategemea ukubwa wa familia au wingi wa wakazi. Kuna wanaofua kila siku, kila baada ya siku au mara moja kwa wiki. Wengine Hufua kwa mashine na kukausha kwa dryer, hawa siwaongelei hapa kwani ni wachache sana.
Nguo kuanikwa hovyo hovyo kunapoteza uzuri wa nyumba. Unakuta ni nyumba nzuri barazani kuna nguo zimeanikwa. Zile za community ndiyo balaa, nguo kuonekana kambani ni sehemu ya maisha.
Kusema ukweli kutegemea nishati ya jua kukaushia nguo ni rahisi na unaokoa pesa pia mazingira. Kutumia umeme kukaushia nguo ni wakati tuna jua la ziada ni matumizi mabaya ya nishati.
Kama unajenga nyumba ni mihimu kufahamu idadi ya watu watakaoishi humo pia huduma zao kama kuanika nguo zitakuaje. Ni nyumba chache za community unakuta kuna makaro ya kufulia na miti na kamba za kuanikia nguo hasa nyuma ya nyumba. Pia unaweza kuvuta bati hasa lile transparent uweke eneo la kuanikia nguo siku za mvua.
Huwa ninakereka kuona maghorofa mazuri mjini lakini barazani nguo zimeanikwa. Uzuri wa nyumba unapotea ghafla.