CompaQ
JF-Expert Member
- Dec 31, 2012
- 281
- 134
wamekuwa wakitafuta taarifa zaidi kuhusu
ulaji wa vyakula mbalimbali siku hadi siku.
Baadhi ya taarifa wanazozipata, zimeonyesha
kuwa na utata, hivyo kuwafanya watu hao
kuwa na maswali mengi yanayohusu ulaji wa
vyakula mbalimbali.
Ni dhahiri kwamba, lishe bora ni moja ya
vipengele muhimu katika kuboresha afya ya
mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI.
Kumekuwa na Maswali yanayoulizwa mara
kwa mara, kuhusiana na hali hii, ili kujibu
baadhi ya maswali yaulizwayo mara kwa
m a r a .
Kutokana na kuongezeka kwa maswali na ari
ya watu hao ya kutaka kujua zaidi juu ya lishe
na ulaji unaofaa ikanibidi niwa andikie makala hii.
MASWALI NA MAJIBU
SWALI:
Je, nyama nyekundu ina madhara gani kwa
mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI?
JIBU:
Kuna nyama za aina mbili, nazo ni nyama nyeupe na nyama nyekundu.
Nyama nyeupe
ni pamoja na samaki, kuku, ndege wa aina
zote, bata, wadudu; na nyama nyekundu ni
pamoja na ng'ombe, mbuzi, kondoo,
nguruwe na wanyama wa porini. Nyama ina
virutubishi vingi muhimu kwa afya ya
binadamu kama protini, vitamini na madini.
Madini ya chuma yanayopatikana kwenye
nyama ni rahisi sana kusharabiwa
(kufyonzwa) mwilini na ni muhimu kwa
kuongeza wekundu wa damu.
Uwezo wa miili ya watu wanaoishi na virusi
vya UKIMWI kuyeyusha chakula na
kusharabu (kufyonza) virutubishi hupungua.
Utumiaji wa nyama nyekundu kwa wingi
unaweza kuwaletea matatizo hasa katika
uyeyushwaji tumboni kwani nyama nyekundu
si rahisi kuyeyushwa ukilinganisha na nyama
nyeupe.
Hata hivyo katika nchi yetu watu walio wengi
wanatumia nyama kwa kiasi kidogo sana na
mara chache. Si vyema watu hawa waache
kabisa nyama nyekundu. Jambo la muhimu ni
kutumia njia mbalimbali ili kuifanya nyama hii
iyeyushwe kwa urahisi tumboni.
Namna ya kusaidia uyeyushwaji ni pamoja
n a : -
• Kutafuna vizuri au kutumia nyama ya
kusaga (kwa wanaoipata).
• Kupika nyama na viungo vinavyosaidia
kulainisha kama vile papai bichi, limao,
vitunguu saumu n.k.
• Kula nyama pamoja na papai
Inashauriwa kwa anayepata nyama nyekundu
kwa wingi, kupunguza kiasi cha nyama hiyo
na kuongeza kiasi cha nyama nyeupe. Na kwa
yule asiyepata nyama nyeupe, apatapo nyama
nyekundu asiache kutumia kwani ina
umuhimu mwilini mwake.
Una weza pia kulainisha vipande vya nyama
mbichi kwa kuigonga-gonga, mpaka ilainike
kabla ya kupikwa.
SWALI:
Je, ni nini tofauti kati ya yai la kuku wa
kienyeji na la kuku wa kisasa?
JIBU:
Kilishe mayai yote ni sawa. Vi r u t u b i s h i
vinavyopatikana kwenye yai la kuku wa
kienyeji kama protini, vitamini A, madini ya
chuma na virutubishi vya aina nyingine,
ndivyo hivyo vinavyopatikana pia kwenye yai
la kuku wa kisasa.
Tatizo linaweza
kutokea pale ambapo wafugaji wa
kuku wa kisasa hawafuati taratibu
za ufugaji na pengine hawawapi
kuku vyakula muhimu
wanavyohitaji, hivyo wakati
mwingine kiini cha yai la kuku wa
kisasa huonekana kupungua rangi ya
njano kuliko kiini cha yai la kuku wa kienyeji.
Mtu anashauriwa kula yai bila kujali ni la
kuku gani, kwa kutegemea ni yai lipi
linapatikana kwa urahisi.
SWALI:
Je, ulaji wa yai bichi una madhara gani?
JIBU:
Yai bichi linaweza kuwa na vijidudu viitwavyo
kwa kitaalamu "SALMONELLA" vinavyoweza
kusababisha tumbo kuuma, kichefuchefu na
pia kuharisha.
Vijidudu ya "Salmonella"
vinaweza kusababisha madhara makubwa
kwa watoto, wazee na wale wenye hali dhaifu
ya kimwili kama wagonjwa wa UKIMWI.
Pia yai bichi lililowazi linaweza kuwa zalio zuri la
vimelea vya maradhi mbalimbali. Inashauriwa
kupika yai mpaka liive kabisa, na kuhakikisha
kwamba hakuna ute unaoteleza. Kama ni yai
la kuchemsha, lichemshwe kwa dakika kumi
zaidi baada ya maji kuchemka. Pia ni muhimu
kuhakikisha kwamba vyombo vilivyotumika
k u k o rogea yai bichi vinaoshwa kwa maji na
sabuni kabla ya kuvitumia tena kwa matumizi
mengine ili kuepuka maradhi.
Ikumbukwe kuwa, mtu anayeishi na virusi
vya UKIMWI amepungukiwa na kinga ya
mwili, kwa hiyo ni muhimu kujiepusha na
chochote kinachoweza kuleta hatari ya
kuambukizwa magonjwa.
SWALI:
Je, unywaji wa soda una madhara gani?
JIBU:
Soda ni kiburudisho ambacho si muhimu sana
kwa afya. Aina nyingi za soda zina kafeini
ambayo huzuia usharabu (ufyonzwaji) wa
madini ya chuma mwilini hasa yatokanayo na
vyakula vya mimea
Hata hivyo soda zinaweza kutumika kwa kiasi
kidogo kama kiburudisho, ila tunapotaka
ubora zaidi wa afya zetu inafaa kupunguza
matumizi ya soda na badala yake kutumia
vinywaji vyenye virutubishi muhimu kama
vile maji ya matunda, maziwa, madafu au
asusa kama vile matunda, karanga na aina
mbalimbali za mboga mfano karoti. Hii
inasaidia pia kutumia fedha kidogo tuliyo
nayo kwa vyakula muhimu, hasa ukizingatia
badala ya soda moja unaweza kupata mayai
matatu au nusu lita hadi lita moja ya maziwa.
SWALI:
Je, matumizi ya chai na kahawa yana madhara
g a n i ?
JIBU:
Kwa kawaida chai na kahawa ni viburidisho
ambavyo huchangamsha mwili, kutokana na
kuwepo kafeini ndani ya vinywaji hivyo,
lakini sio muhimu mwilini. Si vizuri kutumia
vinywaji hivi pamoja na chakula, kwani
kafeini huzuia usharabu (ufyonzwaji) wa
madini ya chuma mwilini, yatokanayo na
vyakula vya mimea.
Kwa kuwa mtu anayeishi
na virusi vya UKIMWI anahitaji madini
hayo, ni bora kupunguza sana
matumizi ya chai na kahawa hasa wakati wa chakula.
Inapobidi kutumia vinywaji hivi, vitumike kwa kiasi
kidogo, na kiasi cha majani au kahawa inayowekwa ndani
ya kinywaji iwe kidogo; na
vitumike angalau saa moja kabla ya chakula au saa moja
baada ya kula.
Ni vizuri kujaribu vinywaji vya aina nyingine
badala ya chai, kwa mfano vile
vinavyotengenezwa kutokana na viungo,
majani ya mchaichai, majani ya mlimao, choya
( rozela), nanaa, tangawizi na vinginevyo.
MAKALA HII ITAENDELEA KWENYE POST ITAKAYOFUATA ENDELEA KUFUATILIA MASWALI NA MAJIBU HAYA
ManyandaHealthy