Sehemu za kuingilia Kigamboni; Kigamboni Ferry na Darajani kufungwe Camera kudhibiti uwezekano wa kuwa eneo la kihalifu

Sehemu za kuingilia Kigamboni; Kigamboni Ferry na Darajani kufungwe Camera kudhibiti uwezekano wa kuwa eneo la kihalifu

Twilumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2010
Posts
12,576
Reaction score
14,522
Kulingana na matukio ambayo yameanza kujitokeza ya uhalifu nazishauri Mamlaka sasa ziwezeshe vifaa vya utambuzi kama Camera kwenye maeneo ya kuingilia kigamboni kwa maana ya Ferry na Daraja la Mwalimu Nyerere ili kwa kiasi kudhibiti matukio ambayo yameanza kujitokeza hasa ukizingatia kuwa Kigamboni ina Maeneo makubwa yenye mapori makubwa na eneo kubwa ambalo lipo karibu na Bahari sehemu ambayo ikiwa nia ya dhati isipokuwepo kunaweza kugeula eneo jipya la utekaji, utesaji na mauaji.

Hii ni kwa sababu eneo la kigamboni ni rahisi kudhibiwa kutokana na Jiografia yake na maeneo ya kuingia maeneo hayo.

Maeneo ambayo yalikuwa yana historia ya kuokotwa watu wakiwa wametekwa na kutelekezwa kama Magwepande yamedhibitiwa kwa gharama kubwa kwa sababu ya jiografia yake kuwa ngumu lakini kwa Kigamboni udhibiti ni rahisi kulingana na Jiografia hiyo.

Ni matumaini yangu kuwa jambo hili litafanywa ikiwa mamlaka zina nia ya kweli ya kulinda Raia wake na kupunguza matukio hasi kwa raia.
 
Back
Top Bottom