Habarindiyohiyo
JF-Expert Member
- Aug 11, 2008
- 263
- 16
king'ang'anizi wa madaraka ni yule anayelazimisha madaraka nje ya kanuni na taratibu, sasa kama Seif anafuata kanuni amabazo chama chenyewe cha CUF waliona zinafaa iweje ahesabike anang'ang'ania madaraka?. kudai kuwa CCM wameshabadilisha kutoka Salmin mpaka Karume ni mfano usiofaa, infact Salmin alitaka abadili katiba ili aendelee, seif yeye hajabadili katiba mahali popote pale ya CUF ili kuji'favour' kugombea uraisi. kitu kingine ni kwamba Seif ni big shot, chance ya kuupata uraisi zenji ni kubwa kuliko mtu mwingine atleast kwa sasa, kwa sababu anafahamika vyema.
anyway tuliangalie hili suala kwa uchambuzi akinifu, Seif hajawahi kuwa raisi, na wala hajawahi kubadili katiba ili impe favour, kwa hiyo siyo king'ang'anizi wa madaraka bali ndo kwanza anaweka juhudi ili ayapate hayo madaraka anayoyataka
anyway tuliangalie hili suala kwa uchambuzi akinifu, Seif hajawahi kuwa raisi, na wala hajawahi kubadili katiba ili impe favour, kwa hiyo siyo king'ang'anizi wa madaraka bali ndo kwanza anaweka juhudi ili ayapate hayo madaraka anayoyataka
Edward si alirudi bana, akashindwa kwenye primaries, Mcain naye alishindwa na Bush kwenye primaries lakini akarudi tena this time,kugombea zaidi ya mara moja kwa mwanasiasa siyo ishu, ishu ni kung'ang'ania madaraka kama Mugabe na Kibaki, au kubadili katiba ili ikupe favor kama MuseveniSeif kachemka,
Huwezi kutoa kauli oxymoronic kama hiyo.Kama kweli wewe huamini katika ung'ang'anizi kwa nini hupishi wengine kugombea? Pengine sababu watu ving'ang'anizi wa CCM wanaendelea kuwapo ni kutokana na wananchi kuona hata upinzani nako kuna ving'ang'anizi, hama mabadiliko, kwa hiyo uchaguzi unakuwa tuchague ving'ang'anizi wa CCM au wa CUF? Mwisho wanaona "Zimwi likujualo halikuli likakwisha".
Wapeni watu vijana wachanga wenye mbinu mpya wapambane na hao ving'ang'anizi halafu tuone kama watabaki.
Si umeona "Change We Can Believe In" ya Obama, wangerudi kina Edwards na Kerry nina shaka hata kama wangeweza kumshinda McCain.
Edward si alirudi bana, akashindwa kwenye primaries, Mcain naye alishindwa na Bush kwenye primaries lakini akarudi tena this time,kugombea zaidi ya mara moja kwa mwanasiasa siyo ishu, ishu ni kung'ang'ania madaraka kama Mugabe na Kibaki, au kubadili katiba ili ikupe favor kama Museveni
Sultan Seif Sharrif Hamad ameshachukua fomu za kugombea tena nafasi ya katibu mkuu wa CUF. Lipumba yeye amesema ataamua wiki moja kabla ya uchaguzi wa chama hicho ili kutowatisha wanachama wengine kuchukua fomu na kugombea.
Sambamba na hilo Seif ametangaza kuwa atagombea tena kwa mara ya nne urais wa Zanzibar. Mwenzie Lipumba bado hasema chochote kuhusu kugombea Urais mwaka 2010.
Akichukua fomu hizo mjini Zanzibar, Seif amewakemea viongozi waafrika kwa kuwa ving'ang'anizi wa madaraka kwa kumnyima uongozi kila aliposhinda Zanzibar mwakaa 95, 00, 05.
.....ndiyohiyo
Sultan Seif Sharrif Hamad ameshachukua fomu za kugombea tena nafasi ya katibu mkuu wa CUF. Lipumba yeye amesema ataamua wiki moja kabla ya uchaguzi wa chama hicho ili kutowatisha wanachama wengine kuchukua fomu na kugombea.
Sambamba na hilo Seif ametangaza kuwa atagombea tena kwa mara ya nne urais wa Zanzibar. Mwenzie Lipumba bado hasema chochote kuhusu kugombea Urais mwaka 2010.
Akichukua fomu hizo mjini Zanzibar, Seif amewakemea viongozi waafrika kwa kuwa ving'ang'anizi wa madaraka kwa kumnyima uongozi kila aliposhinda Zanzibar mwakaa 95, 00, 05.
.....ndiyohiyo
Habari za wakati huu.
Kwanza mfahamu Maalim Seif bado hajatamka kabisa kama atagombea urais 2010 ila alikwenda kuchukua fomu ya ukatibu mkuu wa chama cha CUF.
na kwa mujibu wa katiba ya CUF haijaweka mipaka ya umri au mtu atagombea mara ngapi ukiwa na sifa unachukua fomu na kuomba na baadae mkutano mkuu utakupitisha au kukukataa sasa yeye ametumia nafasi hiyo ya katiba ya chama chake lakini pia mwanachama yeyote anayo haki ya kugombea kama anataka kuchukua fomu na yeye amesisitiza hilo kuwa mwenye kutaka kuchukua fomu achukue bila ya kujali kuwa atapambana na naye kwa sababu kila mwanachama ana haki hiyo, ila kwa kuwa Maalim Seif anaheshimika sana ndio watu wenyewe hujirudisha nyuma na kuacha kuchukua hizo fomu lakini yeye hathubutu kuwakataza kwani kama atafanya hivyo ni kwenda kinyume na katiba ya chama chake.
kuhusu kuwaachia vijana sio vibaya kuwapa nafasi vijana kuongoza au kuchukua nafasi kama hizo lakini mfahamu kuwa vijana wachache ambao wanapopewa nafasi wanaziumia vyema wapo wengi tunawaona walivyokuwa na jazba na hasira na baadae kuharibu mambo na katika siasa za zanzibar hakuna kijana wala mtu mzima ambaye ataweza kutumia busara na hekima kama anavyotumia Maalim Seif jamani jamaa amepewa kipaji si mchezo wewe umeona wapi mtu kuibiwa kura mara tatu tena kwa ushidi vijana wake wanapigwa wanaadhibiwa lakini yeye anawaambia subirini Mungu yupo kwani mkilipiza kisasi mnaweza kuiingiza nchi katika balaa na machafuko. nani anaweza hilo jamani. Maalim mwenyewe ameshafunguliwa kesi akakaa miaka minne anakwenda mahakamani akirudi au hamna kumbukumbu nyinyi.
Maalim hawezi kuacha nafasi maana aliwaahidi watanzania kwamba atawatetea akiwa ndani ya CCM au nje ya CCM atawatetea akiwa ndani ya serikali au nje ya serikali kwa hivyo ahadi hayaitimiza bado mwacheni atimize ahadi yake thena atapumzika.
Issue sio kuwa CUF wakimuweka Maalim watashindwa katika uchaguzi no hata wakichukua mtu ambaye ameletwa kutoka mbinguni kwa CCM kutoa madaraka ni ngumu sana kwa hivyo yeyote atakayekaa madhali sio CCM hashindi kwa maana ya hapewi maana kushinda CUF tokea wakati wa dk salimin inashinda na hakuna hata mtu mmoja ambaye halijui hilo ila kupewa ndio hawapewi na ukiwapata CCM wale wakweli wanakwambia wazi wazi kwamba wao uchaguzi wa zanzibar bila ya wizi CCM hawawezi kushinda kabisa na hilo viongozi wote wa bara wanalijua ila haijafika siku yake tu likadhihirika lakini hakuna lisilo na mwisho kila kitu kina mwisho wake na hilo litajitokeza tu.
mnataka wapewe vijana waanze kupigana mawe kama kenya? nyinyi wacheni mchezo huo wa kitoto mwenye kutaka kuchukua fomu ajiunge na hicho chama na kama mwanachama basi mwache achukue fomu na yeye hajakatazwa.
Ushawahi kujiuliza kwa nini wanaorudia rudia wengi wanashindwa?
Halafu Seif siyo tu "zaidi ya mara moja", Seif amekuwa mgombea wa CUF tangu kianzishwe.
au kuweni specific kwamba Seif anang'ang'ania kugombea, lakini nalo siyo kosa kwa sababu kanuni na sheria na taratibu hazijakataza mtu kugombea mara nyingi, ni part ya demokrasia hiyo,