FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,500
- 8,060
Habari!
Shinikizo jipya sambamba na mashitaka ya kumuondoa madarakani Rais wa Marekani Donald Trump vimeibuka upya na kushika kasi baada ya vurugu zilizozuka hivi karibuni bungeni, Washington DC, ambazo Trump analaumiwa na kushutumiwa kwazo.
Huku hayo yakiendelea, kumekuwa pia na mjadala kuhusu kutumika kwa kifungu cha 25 cha marekebisho ya katiba ya Marekani (25th amendment) dhidi ya Trump, kifungu ambacho kinaweka wazi jinsi Makamu wa Rais na wingi wa mawaziri wanavyoweza kumuondoa rais madarakani pale atakaposhindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa katiba.
Democrats wamekuwa mstari wa mbele kushinikiza kuondolewa kwa Trump madarakani kabla ya muda wake kuisha siku chache zijazo. Baadhi ya viongozi na wanachama wa chama cha Republican nao pia wameonekana kuunga mkono hilo na pia kulaani vikali kitendo cha uvamizi wa bunge.
Mmoja wa viongozi ni Spika wa Baraza la Wawakilishi, Bi Nancy Pelosi, ambaye ofisi yake ilivamiwa na waandamanaji (wahuni), amesema (nanukuu):
Vurumai lililozuka bungeni, Washington DC, hapo jana pia limeondoka na maafisa kadhaa wa serikali ya Trump ambapo baadhi tayari wamekwisha kuachia ngazi huku wengineo kadhaa nao wakitegemewa kufanya hivyo katika wakati ujao.
Msako mkali dhidi ya wale wote waliohusika katika vurugu na uvamizi umeanza ambapo tayari watu kadhaa wamekwisha kukamatwa huku pia shirika la upelelezi la FBI likitoa wito kwa raia wa kuwasilisha taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa wahusika wengine.
Jaribio hili kwa mara nyingine la kumuondoa Trump madarakani kabla ya muda wake kuisha litafanikiwa?
Jawabu la kitendawili hiki tutalipata hapo baadaye na mengine zaidi ya haya tutaendelea kujuzana. So long!

(mwisho wa kunukuu)Trump has committed an assault on our nation and our people. Pence must remove him and invoke the 25th amendment. If they fail to act, we may be prepared to move forward with impeachment. Justice will be done to those who carried out these acts of sedition and cowardice.